Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Vodacom Tanzania Yaripoti Ukuaji Imara Uliochagizwa Na Azma Yake Ya Kugusa Jamii Kwa Mwaka Wa Fedha 2025

  • 3
Scroll Down To Discover

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Vodacom Tanzania, David Tarimo (katikati), Mkurugenzi Mtendaji, Philip Besiimire (kushoto) na  Mkurugenzi wa Fedha,  Hilda Bujiku (kulia), wakizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka ambapo walitangaza matokeo ya kifedha ya mwaka wa fedha 2025 yaliyobainisha ukuaji wa mapato na faida. Tukio hilo limefanyika tarehe 21 Agosti kwenye Makao makuu ya Vodacom Dar es salaam.
Dar es Salaam – Agosti 21, 2025: Kampuni ya Mawasiliano na Teknolojia, Vodacom Tanzania PLC imefanya mkutano wake wa mwaka wa wanahisa kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 31 Machi 2025. Matokeo ya kifedha na kiutendaji yaliyowasilishwa katika mkutano huo yanaonesha ukuaji imara, uwekezaji wa kimkakati na muendelezo wa dhamira yao ya kuwawezesha watu, kulinda mazingira na kudumisha uaminifu katika kila walifanyalo.
Katika mwaka huo, mapato ya huduma za Vodacom yaliongezeka kwa asilimia 20.5 hadi kufikia Shilingi trilioni 1.5, yakichochewa na ongezeko la wateja na matumizi ya huduma zake, hasa M-Pesa na huduma za data. Faida halisi baada ya kodi iliongezeka kwa asilimia 69.4 hadi TZS bilioni 90.5, ikichangiwa na mikakati ya kupunguza gharama iliyookoa TZS bilioni 59. Kampuni iliongeza wateja wapya milioni 3, na hivyo kufikia jumla ya wateja milioni 22.6 mwishoni mwa mwaka.
Mapato ya M-Pesa yaliongezeka kwa asilimia 29.3, huku thamani ya miamala ikiongezeka kwa asilimia 33.8 mwaka hadi mwaka. Matumizi ya simujanja yaliongezeka kwa asilimia 33.4, na hivyo kuchochea upatikanaji wa huduma za kidijitali. Zaidi ya hayo, minara mipya 471 ya 4G ilijengwa, ikiwemo 126 katika maeneo ya pembezoni kwa kushirikiana na serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano Sawa kwa Wote (UCSAF).
Ukuaji wa mapato ya Vodacom ulitokana na huduma bunifu za M-Pesa kwa kushirikiana na washirika wake. Huduma hizi ni pamoja na M-Koba, jukwaa la kuweka akiba kwa vikundi linalohudumia zaidi ya wateja milioni 1.3 na M-Wekeza, bidhaa mpya ya uwekezaji kupitia simu, ambayo ilivutia amana za takribani Shilingi bilioni 25 ndani ya miezi michache tangu kuzinduliwa.
Vilevile, jukwaa la malipo ya kidijitali “LIPA kwa simu” lilichakata zaidi ya Shilingi trilioni 1 kila mwezi, huku mikopo ya muda mfupi na Songesha zikikopesha zaidi ya Shilingi trilioni 3, zilizowasaidia wateja na wafanyabiashara kote nchini. Nguzo nyingine ya ukuaji ilikua mapato ya data ya simu, yaliyoongezeka kwa asilimia 21.6, yakichangiwa na matumizi ya simujanja na uwekezaji katika miundombinu ya mtandao.
“Utendaji wetu mwaka huu unaonyesha nguvu ya mkakati wetu na dhamira yetu thabiti ya kuwaunganisha Watanzania na kesho iliyo bora. Kupitia ubunifu na ushirikiano, tunaziba pengo la kidijitali na kifedha,” alisema Philip Besiimire, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania.
Mkakati wa Vodacom unaoongozwa na dhamira thabiti ya kugusa jamii, uliendelea kubadilisha maisha kupitia teknolojia. Nusu ya watumiaji wa huduma ya M-Koba wakiwa ni wanawake, bidhaa hii ni kidhihirisho cha mchango wa Vodacom katika kuwawezesha wanawake kiuchumi. Vilevile, M-Wekeza imekuwa hatua muhimu katika kuleta usawa wa fursa za uwekezaji na kukuza ujumuishwaji wa kifedha.
“Tunapoadhimisha miaka 25 ya kuleta mabadiliko chanya kwa maisha ya Watanzania, tunaendelea kujikita katika ukuaji endelevu na mabadiliko yanayoongozwa na dhamira yetu. Matokeo yetu yanathibitisha imani ambayo wateja na wanahisa wetu wanayo kwetu,” alisema David Tarimo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Vodacom Tanzania PLC.
Tukiangazia mbele, Vodacom inatazamia mazingira thabiti ya kisheria na itaendelea kuwekeza katika upanuzi wa mtandao, huduma bora kwa wateja na ujumuishwaji wa kidijitali. Kampuni inakazia dhamira yake ya kushirikiana na serikali kuboresha viwango vya maisha kupitia huduma za mawasiliano na upatikanaji wa huduma za kifedha kote nchini.



Prev Post ACT Wazalendo Wafanya Kikao Maalum cha Kamati Kuu Kuhusu Uteuzi wa Mwisho wa Wagombea
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook