Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

HII HAPA TAREHE YA SIMBA, YANGA KUKUTANA MSIMU HUU…

  • 39
Scroll Down To Discover

BODI ya Ligi Tanzania imetangaza mechi za timu nne za juu, Yanga, Simba, Azam na Singida Black Stars, ambazo zitapambana kuwania Ngao ya Jamii, kuanzia Septemba 11 hadi 14 mwaka huu.

Mabingwa wa Tanzania Bara na washindi wa Ngao ya Jamii msimu uliopita, Yanga, itakwaana na Azam FC, huku Simba ikiikabili Singida Black Stars.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Mawasiliano ya Bodi ya Ligi ilitangaza michezo hiyo ya nusu fainali, wakati ikitoa Kalenda ya Matukio na Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa msimu wa 2025/26.

Ndani ya kalenda hiyo, bodi hiyo imeweka michezo ya Ngao ya Jamii kuchezwa, Septemba 11 hadi 14 itakapochezwa fainali, huku Ligi Kuu Tanzania Bara ikianza kutimua vumbi, Septemba 16 mwaka huu.

Ingawa bado haijatoa ratiba na tarehe rasmi za michezo hiyo, lakini kwa mujibu wa kanuni ni kwamba bingwa wa Ligi Kuu anatakiwa kucheza na mshindi wa tatu, huku wa pili akicheza na timu iliyomaliza nafasi ya nne kwenye ligi.

Yanga iliyomaliza nafasi ya kwanza, itacheza na mshindi wa tatu, Azam FC, katika mechi ya kulipizana kisasi ya kile kilichotokea Ligi Kuu msimu uliopita.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa, Novemba 2, mwaka jana, Azam ilishinda bao 1-0, lakini mzunguko wa pili wa Ligi Kuu, uliishuhudia Yanga ikishinda mabao 2-1, Aprili 10, mwaka huu, hivyo kila mmoja atataka kulipa kwa mwenzake.

Mshindi wa pili, Simba, itakutana na Singida, iliyomaliza nafasi ya nne, huku Simba ikitaka kwenda kulipa kisasi kwa kile ilichofanyiwa, Mei 31, mwaka huu, ilipotandikwa mabao 3-1, katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA, Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati, Manyara.

Simba ilipata ushindi wa bao 1-0 mara mbili kwenye michezo ya Ligi Kuu, kabla ya kukutana na dhahama hiyo.

Timu zitakazoshinda michezo hiyo, zitakwenda hatua ya fainali itakayopigwa, Septemba 14, mwaka huu.

The post HII HAPA TAREHE YA SIMBA, YANGA KUKUTANA MSIMU HUU… appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post Utalii Wafunga Mwaka 2024/25 Ukiongoza Fedha za Kigeni
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook