Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

A-Z JINSI CHIKOLA ALIVYOTUA YANGA KWA ‘MZAHA’ WA ENG HERSI….

  • 36
Scroll Down To Discover

WINGA, Offen Chikola, amesema kwake itakuwa rahisi kujitangaza na kupata soko la kucheza la kulipwa nje ya Tanzania baada ya kujiunga na Yanga.

Yanga juzi ilitangaza kukamilisha usajili wa Winga huyo wa zamani wa Tabora United.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Chikola, alisema hata alipopigiwa simu kwa mara ya kwanza na Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, kwake ilikuwa kama ndoto, kwani kwa uwezo wake alikuwa anatamani acheze kwenye klabu ambayo inaonekana zaidi kwenye michezo ya kimataifa kwa ajili ya kujitangaza zaidi.

“Hersi, aliongea kama utani hivi, unataka kuendelea kucheza kwenye klabu zako hizo za huko?, lakini ukweli hata mimi mwenyewe nilitamani kucheza klabu kubwa kwa sababu timu nyingine ningechelewa sana kuonekana,” alisema Chikola.
Akizungumzia kuwa sehemu ya klabu hiyo, Chikola, alisema anajisikia vizuri kuvaa jezi ya Yanga na kuahidi kuipambania ili kuzidi kuipa mafanikio.

“Najisikia vizuri sana, nina furaha kubwa sana kuvaa jezi ya Yanga kwa sababu ni ndoto ya kila mchezaji wa hapa nchini au nje ya nchi kuvaa nembo hii.

Mpaka nimesajiliwa, viongozi wameona kuna kitu naweza kukiongeza kwenye kikosi, binafsi mimi nachukua kama fursa, nina ari ya kuipambania klabu hii. Nilikuwa kwenye ligi ambayo Yanga ilikuwemo, naitambua timu hii jinsi ilivyo na najua ina wachezaji wakubwa na bora kabisa hapa Afrika,” alisema.

Hata hivyo, alisema hatoangalia ubora wa mchezaji yoyote ndani ya timu hiyo ila atakachoangalia zaidi ni ubora wake ambao utaongeza kitu kwa ajili ya malengo ya klabu.

“Nitaangalia zaidi ubora wangu mimi mwenyewe ambao utaongeza kitu kwa ajili ya kuipambania klabu, nipo tayari kushirikiana na wenzangu wote watakaokuwepo ili tutimize malengo ya klabu,” alisema.

Katika hatua nyingine, Chikola, alifichua kuwa ameamua kuendelea kuvaa jezi namba 31 aliyokuwa akiivaa akiwa Tabora United msimu uliopita kwa sababu ana bahati nayo.

“Nimeamua kuendelea na jezi namba 31 niliyokuwa naivaa nikiwa Tabora United kwa sababu naona msimu uliopita ulikuwa mzuri sana kwangu nikiwa na jezi hii, sikuwahi huko nyuma kuvaa namba hii, lakini tangu nilipofanya hivyo msimu uliopita, nimekuwa na bahati nayo,” alisema.

Chikola, alimaliza Ligi Kuu msimu uliopita akiwa na mabao saba, ambapo mechi iliyomfanya atambulike zaidi ni ile ya Tabora United dhidi ya Yanga iliyocheza, Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa, Novemba 7, mwaka jana, licha ya kuwanyanyasa mabeki wa Yanga, Chikola alifunga mabao mawili, dakika ya 19 na 45, akiiongoza Tabora United kupata ushindi wa mabao 3-1.

Mabao mengine katika mchezo huo yalifungwa na Nelson Munganga kwa upande wa Tabora United huku la kufutia machozi la Yanga likifungwa na Clement Mzize.

The post A-Z JINSI CHIKOLA ALIVYOTUA YANGA KWA ‘MZAHA’ WA ENG HERSI…. appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post Majaliwa: Tuhakikishe Vijana Wanapata Mafunzo Ya Ufundi Stadi
Next Post NAFASI Za Kazi Azam Media, Ajira Mpya Azam TV
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook