Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kada Chipukizi Neto Kapalata Amshinda Kigwangalla Kura za Maoni Nzega Vijijini

  • 40
Scroll Down To Discover

Katika tukio la kisiasa lililoibua mjadala mkubwa, Kada wa CCM Jimbo la Nzega Vijijini, Ndugu Neto Kapalata, ameibuka mshindi katika kura za maoni kwa kupata kura 2,570, akimshinda aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Dkt. Hamis Kigwangalla, ambaye alipata kura 1,715.

Katika mchakato huo, CPA Robert Masegere naye aliibuka na kura 1,635, akifuata kwa karibu nyuma ya Kigwangalla, hali inayoashiria ushindani mkubwa kati ya wagombea watatu hao.

Ushindi wa Kapalata umetafsiriwa na wachambuzi wa siasa kuwa ni “jambo la kustaajabisha mithili ya mende kuangusha kabati”, ikizingatiwa uzoefu, ushawishi na nafasi ya Kigwangalla ndani ya chama na katika siasa za kitaifa.

Matokeo haya yanaweza kuwa na athari kubwa katika sura ya siasa za Nzega Vijijini, na yanaashiria mabadiliko ya mitazamo miongoni mwa wajumbe wa CCM katika ngazi ya jimbo.



Prev Post Shigongo Aongoza Kura za Maoni Buchosa, Tizeba Aambulia Kata Chache
Next Post HUKO YANGA FOLZ AANZA NA MGUU HUU….KWA HILI LAZIMA MASTAA WAPYA WAKIONE CHA MOTO..
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook