Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Magereza Yakanusha Kumsukuma Lissu, Yatoa Maelezo Rasmi

  • 47
Scroll Down To Discover

Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Tundu Antiphas Lissu

Jeshi la Magereza Tanzania limekanusha vikali madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Tundu Antiphas Lissu, yaliyotolewa na mawakili wanaomwakilisha wakiongozwa na Wakili Rugemeleza Nshala, likieleza kuwa Lissu hakusukumwa bali alielekezwa na kuongozwa kwa mujibu wa taratibu.

Katika taarifa kwa umma iliyotolewa na Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Magereza, Jeshi hilo limeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Julai 30, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya mahakama kuahirisha kesi inayomkabili Lissu. Askari wa Jeshi hilo walimwelekeza mahabusu huyo kutoka mahakamani kuelekea gerezani, baada ya kuonesha dalili za kukaidi maelekezo.

“Jeshi la Magereza ni chombo cha Ulinzi na Usalama chenye jukumu la msingi la kuhakikisha usalama wa Mahabusu na Wafungwa wote walio chini ya himaya yake wakiwa ndani au nje ya maeneo ya magereza. Hii inajumuisha kuwalinda dhidi ya madhara yoyote yanayoweza kutokea nje au kusababishwa na wao wenyewe”, imeeleza sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na SACP Elizabeth G. Mbezi, Msemaji wa Jeshi la Magereza siku ya Jumamosi.

Kuhusu baadhi ya askari kujifunika nyuso (maarufu kama ‘Ninja’), Jeshi hilo limefafanua kuwa mavazi hayo hutumika kulingana na mazingira ya kazi au tathmini ya kiusalama kwa lengo la kulinda usalama wa wahusika wote wakiwemo askari, mahabusu na wafungwa.

Aidha, Jeshi hilo limesisitiza kuwa kila mfungwa au mahabusu anapaswa kutii maelekezo ya kisheria bila upinzani wowote. Limeonya kuwa halitasita kuchukua hatua za kiusalama kwa wakati pale panapojitokeza viashiria vya kukaidi au kuvuruga utaratibu.

“Usalama wa Mahabusu Tundu Lissu utaendelea kuimarishwa wakati wote atakapokuwa chini ya mamlaka ya Jeshi la Magereza”, taarifa imehitimisha.



Prev Post TRA Yatoa Msamaha wa Kodi kwa Magari Yasiyokidhi Matakwa ya Forodha
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 03, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook