
Maria Sebastian mkazi wa Jimbo la Kawe Jijini Dar na Kada mwaminifu wa Chama cha Mapinduzi ni mwanamke mwenye elimu ya juu lakini amekuwa akiitumia elimu hiyo katika kujitolea kwa shughuli mbalimbali za kukijenga chama hicho kwa muda mrefu sasa.
Kuhusu elimu yake, Maria ana Shahada ya Uzamili katika Utawala wa Biashara kwenye Mashirika ya Umma na Stashahada ya Juu katika Uendeshaji wa Benki na Fedha kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe na Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (Institute of Finance Management).
Pamoja na elimu hiyo, Maria amepata uzoefu kwa kufanyakazi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kama mchambuzi yakinifu wa biashara ya benki na mifumo ya usalama.
Kwa elimu hiyo ambayo ingeweza kumpa ajira bora kabisa popote ulimwenguni lakini kwa muda mrefu sasa Maria anafanyakazi ya kujitolea katika Chama cha Mapinduzi na jamii kwa ujumla katika kuwawezesha wananchi kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Kwa mustakabali huo Maria sasa amechukua fomu ya kutia nia ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Kawe ili akawapambanie bungeni wananchi wa jimbo hilo na jina lake limerudi sambamba na watia nia wengine saba wote wanaume mwanamke akiwa peke yake.
Hivyo basi Maria amesema anawaomba wajumbe wa CCM na viongozi wa juu wa chama hicho kulipitisha jina lake kama mgombea pekee ili akawapambanie wananchi wa jimbo hilo katika harakati za kimaendeleo endelevu (Sustanable Development). IMEANDIKWA NA RICHARD BUKOS WA GLOBAL PUBLISHERS.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!