Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

NAFASI Za Kazi Chama Cha Ushirika Kagera Kahawa SACCOS Ltd

  • 42
Scroll Down To Discover

NAFASI Za Kazi Chama Cha Ushirika Kagera Kahawa SACCOS Ltd

NAFASI Za Kazi Chama Cha Ushirika Kagera Kahawa SACCOS Ltd

NAFASI Za Kazi Chama Cha Ushirika Kagera Kahawa SACCOS Ltd

Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo KAKASA Ltd (KAGERA KAHAWA SACCOS LTD) ni asasi ya kifedha inayohudumia Wanachama wake ambao ni vyama vya Ushirika wa Kilimo na Masomo (AMCOS) katika wilaya za Halmashauri za Manispaa Bukoba na Bukoba Vijijini, Muleba, na Missenyi katika Mkoa wa Kagera.

Bodi ya Chama hicho inatangaza nafasi ya kazi ya Afisa Mikopo ambayo mwombaji anatakiwa awe Mtanzania yeyote mwenye sifa zinazojitosheleza ili kujaza nafasi hiyo katika Ofisi za Chama zilizopo Mtaa wa Pwani, Kata ya Miembeni, Jengo la Ofisi ya Chama Kikuu cha Kagera Cooperative Union (KCU 1990 Ltd) Manispaa ya Bukoba.

Nafasi inayotangazwa ni:-

✅NAFASI YA AJIRA: AFISA MIKOPO WA CHAMA – 1

SIFA ZA MWOMBAJI NA UZOEFU

  • Awe na Stashahada au Shahada ya kwanza katika fani za Fedha, Uhasibu, Uchumi, Biashara, Masoko au Menejimenti ya Ushirika, huduma ndogo ndogo za fedha au shahada nyingine yoyote inayoendana na sekta ya Fedha husika kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.
  • Awe na uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja, mwenye miaka miwili (2) atakuwa na sifa ya ziada katika SACCOS au kutoka Taasisi za huduma ndogo za fedha.
  • Awe na uwezo wa kuandika na kuongea kwa ufasaha lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
  • Awe na uwezo wa kutumia Komputa kikamilifu na Mifumo ya TEHAMA.
  • Awe na uwezo wa kujituma na kufanya kazi bila kutegemea mtu mwingine. Awe mbunifu katika kuendeleza Chama.
  • Awe anajua kuendesha pikipiki awe na leseni iliyo hai, kwaajili ya kuwatembelea wateja huko vijijini.

KAZI NA MAJUKUMU YA AFISA MIKOPO:-

  • Kuwapokea Wanachama wanaotaka kukopa, kusikiliza nia zao na kuwashauri.
  • Kuwaongoza katika kujaza Fomu za Mikopo kwa usahihi na ukamilifu.
  • Kusimamia, kushuhudia na kuhakiki utiaji sahihi kwa kila mhusika katika Fomu za Mikopo, (kuhakikisha mtia saini ni mhusika halisi na si mtu mwingine).
  • Kuhakiki, na kukagua uhalali wa umiliki wa Mali inayowekwa kuwa Dhamana ya Mkopo, ubora wake, na thamani (monetary value) ya Dhamana Mwanachama Mkopaji au Mdhamini wa Mkopaji.
  • Upokeaji wa Maombi ya Mikopo -Kupokea na kuhakiki nyaraka za maombi ya mikopo kutoka kwa wateja na kuhakikisha kuwa wateja wamekidhi vigezo vya awali vya kupata mkopo.
  • Kuzipeleka Fomu Mikopo zilizokamilika kwa Mhasibu kwaajili ya uhakiki wa Taarifa za kifedha zilizojazwa humo na kupata maoni ya Mhasibu na baadae kwa Meneja kupata maoni yake (kabla ya kuzifikisha kwenye Kamati ya Mikopo kwa uamuzi).
  • Tathmini ya Mikopo – Kufanya uchambuzi wa kina wa maombi ya mikopo, akiwa ni pamoja na uwezo wa mkopaji kulipa na kutumia zana kama ripoti za mikopo, dhamana (collateral), na historia ya kifedha ya mteja.
  • Kuzipeleka Fomu za Mikopo zilizokamilika kwenye Kamati ya Mikopo kujadiliwa zikiambatana na Hati za Dhamana za Mkopo husika.
  • Utoaji wa Mapendekezo – Kutoa mapendekezo kwa kamati ya mikopo au menejimenti juu ya maombi ya mikopo yanayopaswa kuidhinishwa au kukataliwa.
  • Kuzipeleka Fomu za Mikopo zilizopitishwa na zilizokataliwa kwa Meneja ambaye baadaye atazipeleka kwa Mhasibu na zilizokataliwa atatoa mwongozo kwako.
  • Utoaji wa Mikopo kuhakikisha mikopo iliyopitishwa imetolewa kwa wanachama kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na kuthibitisha makubaliano ya mkopo na kuhakikisha mteja anaelewa masharti ya mkopo.
  • Ufuatiliaji wa Mikopo – Kufuatilia marejesho ya mikopo ili kuhakikisha kuwa wateja wanalipa kulingana na makubaliano ya mkataba na Kushughulikia mikopo isiyiolipwa kwa wakati na kuchukua hatua za kurejesha fedha na kushauri hatua za kuchukua kwa mkopo chechefu (non-performing loans).
  • Kumsimamia Mkusanyaji wa Madeni ya chama na kufuatilia Mashauri ya Kesi zilizopo Mahakamani.
  • Kutembelea miradi ya Wakopaji, kuwashauri na kutoa taarifa za Miradi ya Wakopaji kwa Meneja.
  • Ushauri /elimu kwa wateja – kuwashauri wateja juu ya masuala ya kifedha, ikiwa ni pamoja na mipango ya kulipa mikopo na kuboresha hali zao za kifedha na kuwaelimisha juu ya bidhaa na huduma za kifedha zinazotolewa na taasisi. maombi.
  • Utawala wa Kumbukumbu kudumisha kumbu kumbu sahihi za marejesho, na hali ya mikopo ya wateja na kuandaa ripoti za utendaji wa mikopo kwa menejimenti.
  • Kuzingatia sheria, na Kanuni na sera ya mikopo kuhakikisha kuwa shughuli zote za utoaji wa mikopo zinazingatia sheria za nchi na sera za taasisi na kuweka viwango vya juu vya uadilifu na usiri.
  • Kusaidia katika ukuzaji wa SACCOS – Kushirikiana na wanachama kutambua mahitaji ya kifedha yanayoweza kusaidia ukuaji wa SACCOS na kupendekeza maboresho ya huduma za mikopo ili kuvutia wanachama wapya.

Kufanya kazi nyingine utakazopangiwa na Meneja.

Katika nafasi hii utawajibika kama AFISA MIKOPO

NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
Kwa yeyote mwenye sifa awasilishe barua ya maombi yake ikiambatana na nakala zilizothibitishwa za vyeti vya elimu na taalua. Cheti cha kuzaliwa, nakala ya kitambulisho cha uraia (NIDA), Nakala ya leseni ya Udereva ambayo haijaisha muda wake na wasifu binafsi wa mwombaji (CV) wenye anuani, mawasiliano na majina, anwani na namba za simu zinazopatikana za wadhamini.

Maombi yote yaletwe ofisini au yatumwe katika anuani ifuatayo:-
Kupitia e-mail ya Chama: kagerakahawasaccosltd@yahoo.com
Au
MWENYEKITI WA BODI,
KAGERA KAHAWA SACCOS LTD, S.L.P. 05,
BUKOBA KAGERA

Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 28/08/2025 Saa 9.30 mchana.



Prev Post NAFASI Za Kazi CRDB Bank PLC
Next Post NAFASI za Kazi DP World
Related Posts
© Image Copyrights Title

NAFASI za Kazi SJUT Tanzania

© Image Copyrights Title

NAFASI Za Kazi Barrick Gold Mine

Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook