

Mtia nia wa ubunge Jimbo la Missenyi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Evance Kamenge, amewapongeza madiwani wa viti maalum waliochaguliwa katika uchaguzi wa ndani wa chama uliofanyika Julai 20, 2025, huku akitoa wito kwa wanachama wote kuendeleza mshikamano na ushirikiano kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza na vyombo vya habari, Kamenge alieleza kuwa kipindi hiki cha uchaguzi ni fursa kwa kila mwanachama kunufaika, hivyo ni muhimu kushirikiana kwa pamoja ili kufanikisha maendeleo ya kweli kwa wananchi wa Missenyi.
Aidha, Kamenge aliwatia moyo wale ambao hawakupata nafasi ya kuteuliwa kuwa madiwani wa viti maalum, akiwahimiza kuendelea kuhudumia jamii katika nafasi walizonazo na kusubiri fursa nyingine zijazo.
Kwa sasa, Kamenge anasubiri mchakato wa uteuzi wa wagombea wa ubunge kupitia CCM, huku akisisitiza kuwa endapo atapata nafasi hiyo, atakuwa kiongozi wa vitendo na atawajibika kwa wananchi kwa njia inayoonekana.
“Nina dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Missenyi vipaumbele vyangu vitakuwa katika uchumi wa uzalishaji na maendeleo ya jamii,” alisema Kamenge.
Kamenge ambaye ni Mchumi na mkulima
ametoa wito kwa wanachama wote wa CCM Missenyi kuendelea kushikamana na kuunga mkono juhudi za chama kupitia Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Dkt Samia Suruhu Hassani katika kuleta maendeleo kwa wananchi.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!