Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

CCM Yatangaza Tarehe ya Kura ya Maoni kwa Ubunge na Udiwani Kufanyika Agosti 4, 2025

  • 43
Scroll Down To Discover

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza rasmi kuwa kura za maoni kwa wagombea wa nafasi za Ubunge, Udiwani na Uwakilishi zitafanyika Agosti 4, 2025, kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa ya chama, wagombea wote waliorejesha fomu na kupita hatua za awali watapigiwa kura na wajumbe wa mikutano mikuu ya kata, wadi na majimbo, ambapo kila nafasi itawasilishwa kwa wanachama kwa njia ya kidemokrasia.

CCM imesisitiza kuwa uteuzi rasmi wa wagombea utatekelezwa mwishoni mwa mwezi Agosti, kupitia viongozi wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa, kwa kuzingatia amani, uwazi na heshima kwa taratibu za chama.

Lengo kuu ni kupata wagombea bora, waadilifu na wenye uwezo wa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi katika ngazi zote za uongozi.



Prev Post Majaliwa Akutana Na Waziri Mkuu Wa Belarus, Wasaini Makubaliano Muhimu Ya Ushirikiano
Next Post Kamenge: WanaCCM Tuwe Wamoja Kuelekea Uchaguzi
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook