Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Ajali Ya Ndege Ya Kijeshi Yauwa 19 Dhaka, Bangladesh

  • 54
Scroll Down To Discover

Watu 19 wamefariki dunia na wengine 164 kujeruhiwa baada ya ndege ya mafunzo ya Jeshi la Anga la Bangladesh kuanguka kwenye jengo la shule ya Milestone School and College iliyopo eneo la Uttara, Dhaka – Bangladesh.

Kwa mujibu wa Jeshi la Anga, ndege hiyo aina ya F-7 ilipata hitilafu ya kiufundi muda mfupi baada ya kuruka kwa ajili ya mazoezi saa 7:00 mchana kwa saa za huko. Rubani wa ndege, Flight Lieutenant Md. Taukir Islam, ni miongoni mwa waliopoteza maisha.

Taarifa zinaeleza kuwa zaidi ya 50 kati ya waliojeruhiwa ni watoto na watu wazima waliopata majeraha ya moto, na wamepelekwa hospitalini kwa matibabu.

Mashuhuda wamesema waliona ndege hiyo ikigonga jengo la shule moja kwa moja, na kusababisha mlipuko mkubwa ulioambatana na moto na moshi mzito.

Kiongozi wa Serikali ya Mpito, Muhammad Yunus, ametangaza siku ya maombolezo Jumanne, na kueleza kuwa uchunguzi umeanza mara moja ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.



Prev Post Rais Samia Aridhia Tanzania Kuandaa Miss World 2027
Next Post PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO JULAI 22, 2025
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook