Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi, Usimamizi na Utawala bora wa elimu katika shule kwa maafisa elimu kata Tanzania bara yaliyofanyika ADEM halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi, Usimamizi na Utawala bora wa elimu katika shule kwa maafisa elimu kata Tanzania bara yaliyofanyika ADEM halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Maulid J. Maulid akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi, Usimamizi na Utawala bora wa elimu katika shule kwa maafisa elimu kata Tanzania bara yaliyofanyika ADEM halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani.

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeendelea kuimarisha uongozi na usimamizi wa elimu nchini kwa kutoa mafunzo ya uongozi, usimamizi na utawala bora kwa walimu wakuu wa shule za awali na msingi pamoja na maafisa elimu kata kutoka Tanzania Bara.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika ADEM, Julai 9, 2025 Bagamoyo mkoani Pwani, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo amesema mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha viongozi wa elimu kusimamia kwa ufanisi shughuli mbalimbali za shule ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu, uimarishaji wa mazingira salama ya kujifunzia na kuongeza uandikishaji wa wanafunzi.
“Mafunzo haya ni sehemu ya jitihada za Serikali kuhakikisha kwamba viongozi wa elimu wanakuwa na uwezo wa kiutendaji na kiuongozi katika kuhakikisha elimu bora inatolewa nchini,” amesema Prof. Nombo.
Aidha, amebainisha kuwa Wizara kupitia Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), itaendelea kutoa mafunzo endelevu kwa viongozi wa elimu wa ngazi mbalimbali pamoja na wadau wa elimu ili kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa shule kwa ufanisi.
“Matumaini yetu ni kwamba ADEM itaendelea kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa lengo la kuimarisha uongozi wa elimu kwa njia endelevu na yenye tija,” ameongeza .
Baadhi ya maafisa elimu kata wakiwa katika ufunguzi wa Mafunzo ya Uongozi, Usimamizi na Utawala bora wa elimu katika shule kwa maafisa elimu kata Tanzania bara yaliyofanyika ADEM halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo (katikati) akiwa naMwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Leonard Akwilapo (wa tatu kulia),Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Maulid J. Maulid pamoja viongozi wengine wakiwa kwenye picha ya pamoja
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dkt. Maulid J. Maulid amesema awamu ya kwanza ambayo imezinduliwa leo (Julai 9, 2025) kitaifa, imejumuisha mikoa 12 yenye washiriki kutoka mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Dodoma, Lindi, Mbeya, Arusha, Pwani, Morogoro, Iringa, Njombe, Mtwara na Singida.
Amesema walishafanya mafunzo kwa wakuu wa shule 17,817, na sasa mafunzo hayo yatafanyika kwa maafisa elimu kata 3956.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!