Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Majaliwa Azindua Mitambo Ya Shillingi Billioni 12.4 Kwa Ajili Ya Wachimbaji Wadogo

  • 39
Scroll Down To Discover

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akiwasili eneo la tukio

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua mitambo kumi ya uchorongaji na vifaa vya utafiti wa madini yenye thamani wa shilingi bilioni 12.41 kwa ajili ya wachimbaji wadogo ambayo itapunguza changamoto za wachimbaji wadogo ya kufanya uchimbaji bila kuwa na taarifa za kijiolojia.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo uliofanyika leo Jumanne (Juni 24, 2025) kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa hatua hiyo ni mwendelezo wa juhudi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuboresha shughuli za wachimbaji wadogo wa madini na kuwawezesha kuongeza uzalishaji.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akipokea maelezo kutoka kwa wataalamu kuhusu mitambo ya uchorongaji na vifaa vya kisasa vya utafiti vilivyolengwa kuwawezesha wachimbaji kuongeza tija na usalama katika shughuli za madini, wakati wa uzinduzi rasmi Juni 24, 2025.

“Oktoba 2023 Rais Dkt. Samia, alizindua mitambo mitano ya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo. Kutokana na wingi wa wachimbaji wadogo nchini na mwitikio chanya wa wachimbaji wadogo alielekeza Wizara ya Madini kuongeza mitambo mingine”

“Mitambo hiyo mitano imeshatoa huduma ya uchorongaji kwa wachimbaji 16 katika maeneo mbalimbali nchini na kuchoronga jumla ya mita 3,450.37”

Kadhalika Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa kuongezeka kwa mitambo ya uchorongaji maalumu kwa wachimbaji wadogo kutaleta mageuzi na manufaa makubwa katika sekta madini. “Moja ya faida kubwa za mitambo hiyo, ni pamoja na kuongeza chachu ya ukuaji wa shughuli za wachimbaji wadogo nchini kwa kuwa itawawezesha upatikanaji wa taarifa za uhakika za jiolojia”

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akikabidhiwa funguo ya heshima kama ishara ya kufungua rasmi mitambo ya uchorongaji na vifaa vya utafiti, katika uzinduzi uliofanyika Juni 24, 2025

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa wachimbaji wadogo kuendelea kuuza madini katika viwanda vya ndani vya kusafisha dhahabu ili kuendelea kuchochea ukuaji wa uchumi nchini. “Na wale ambao wanashughulika na usafishaji wa madini, nendeni mkauze kwenye masoko yetu 43 yaliyopo na vile vituo 109, hakikisheni mzunguko wa madini unaanza kunufaisha Taifa letu badala ya kutorosha madini, kama kweli wewe ni mzalendo wa Taifa hili, popote utakapozalisha madini nenda kwenye masoko ya ndani ya nchi.”

Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema kuwa katika mwaka huu wa fedha unaoishia, Sekta ya Madini imefanikiwa kuchangia katika mfuko mkuu wa Serikali kiasi cha shilingi trilioni 1.01. “Pamoja na maboresho haya, kwasasa katika benki Kuu ya Tanzania inahifadhi ya tani 5.7 na kuifanya Tanzania kuwa ndani ya kumi bora ya nchi zenye hifadhi ya dhahabu Afrika”.

Aidha, ameongeza kuwa katika miaka miaka ya minne ya Rais Dkt. Samia madarakani, sekta ya madini imeshuhudiwa ikifanya mapinduzi makubwa ikiwemo kuongeza mchango wake katika pato la taifa ambapo mpaka sasa inachangia asilimia 10.1 kabla ya mwaka wa kimalengo kufika

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa mitambo ya uchorongaji na vifaa vya utafiti kwa wachimbaji, akisisitiza dhamira ya serikali katika kuimarisha sekta ya madini na kuwawezesha wachimbaji wadogo nchini.

Naye, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), John Bina ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia kwa uamuzi wake wa kuamua kuisimamia sekta ya madini ikiwemo kuwawezesha wachimbaji wadogo nchini.

“Madini ni sayansi na madini ni biashara, kwa maboresho haya, sasa watanzania wanachagamkia fursa katika sekta ya madini, wachimbaji sasa wanatosha kuchimba, wachimbaji wadogo tupo pamoja na Serikali yetu, hakika imetuheshimisha.”

Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.



Prev Post Gen Z Warejea Mitaani Kenya Wapaza Sauti Upya Dhidi ya Ukatili wa Polisi
Next Post Askari wa Jeshi la Magereza Kizimbani kwa Kosa la Kumlawiti – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook