Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kesi ya Uhaini Yazidi Kupamba Moto, Lissu Asema Ananyimwa Haki Gerezani – Video

  • 29
Scroll Down To Discover

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Franco Kiswaga, ametoa uamuzi mdogo katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Tundu Lissu ambayo ni kumruhusu Lissu kukabiliana moja kwa moja na Mawakili upande wa Jamhuri na si Mawakili wake kufanya hivyo mpaka atakapoamua vinginevyo.

Uamuzi huo umetolewa muda leo wakati kesi hiyo ikiendelea baada ya Lissu kuieleza Mahakama juu ya madai ya yeye kutotendewa haki akiwa gerezani Ukonga.

“Kwa haya ambayo nimeyasema mawakili wangu nawashukuru, walipambana sana, walipigana kitaalamu, mlifanya majukumu yenu na mliyafanya kwa usahihi. Hivyo ninaichukua kesi hii mikononi mwangu tena. Kwahiyo Mheshimiwa ‘from now on’ mimi ndiye nitakaojibizana na hao mawakili wa serikali”, ameeleza Lissu.

Akijieleza zaidi Lissu alisema “Ninakaa wapi? Gerezani, Gereza la Ukonga kuna sehemu moja inaitwa ‘special room’ eneo maalum ambalo wanakaa wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa, mimi ninakaa hiyo sehemu wanayokaa wanaosubiri kunyongwa ‘death row.

Sasa Mheshimwa ukiwa death row maana yake ni nini? Kanuni ya 33 inazungumzia watu walio death row inasema hivi…ukikaa death row Mheshimwa kama ninachokaa mimi wakati sijahukumiwa kifo angalau bado sheria inasema wale waliohukumiwa kifo wanatakiwa watenganishwe na wafungwa wengine, mimi nimekaa death row tangu Ijumaa Kuu mpaka leo, na nikitoka kuonana na mawakili wangu au ndugu zangu ninaambatana na askari wawili muda wote kama inavyotakiwa kwa waliohukumiwa kifo..Ninalindwa muda wote, usiku na mchana, mimi sijahukumiwa kifo lakini ninakaa death roll pamoja na kuwa death row bado una haki kwa mfano, haki ya kuabudu”, amesema Lissu.

STORI NA ELVAN STAMBULI, GPL



Prev Post Majaliwa: Wakuu Mikoa Hamasisheni Wananchi Kutumia Huduma Za Msaada Wa Kisheria
Next Post Rais Samia: Wasichana Wasome Sayansi kwa Ajili ya Maendeleo ya Taifa – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook