Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

TAMISEMI Yatangaza Uvunjwaji wa Mabaraza ya Halmashauri Ifikapo 20 Juni 2025

  • 38
Scroll Down To Discover

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa ametangaza kwa Vyombo vya habari kuwa Mabaraza yote ya Halmashauri yanapaswa kuvunjwa ifikapo Tarehe 20/06/2025.

Taarifa ya Waziri Mchengerwa imebainisha kuwa ukomo wa Kamati zote za Halmashauri zinazoundwa na Madiwani wa Halmashauri zote nchini utakuwa ni Tarehe 20/06/2025.

“Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri husika ndiye atakayekuwa Mwenyekiti wa mpito wa Halmashauri akisaidiwa na Wakuu wa Idara kama sehemu ya Kamati hadi hapo Uchaguzi utakapofanyika.” Imesema taarifa ya waziri Mchengerwa.

Kulingana na TAMISEMI, hakuna Diwani atakayeendelea na majukumu yake mara baada ya Tarehe 20/06/2026.



Prev Post Puma Energy Tanzania Yadhamini Mkutano wa Wadau wa Ukuaji wa Sekta ya Anga Afrika 2025
Next Post Dkt. Akinwumi Adesina Amaliza Ziara ya Siku 4 Nchini Tanzania
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook