Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mfahamu Jaji Mkuu Mpya wa Tanzania George Masaju

  • 30
Scroll Down To Discover

Jaji wa Mahakama ya Rufani George Mcheche Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania

Juni 13, 2025 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alimteua Jaji wa Mahakama ya Rufani George Mcheche Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania akichukua nafasi ya Prof. Ibrahim Juma aliyemaliza muda wake. Je, Jaji Masaju ni nani?

George Mcheche Masaju ni msomi na mwanasheria maarufu kutoka Tanzania, aliyewahi kushikilia nyadhifa kadhaa muhimu katika serikali.

Awali alianza kazi yake kama Mshauri wa Sheria kwa Rais, kabla ya kuteuliwa na Rais wa Zamani wa Tanzania, Jakaya Kikwete kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Deputy AG) mwaka 2009.

Alishawahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Attorney General): Kikwete alimteuwa rasmi tarehe 2 Januari 2015 na kumuapisha tarehe 5 Januari 2015, kuchukua nafasi ya Frederick Werema aliyejiuzulu baada ya mzozo wa Escrow. Aliendelea kuhudumu pia chini ya Rais Magufuli, hadi kufikia 1 Februari 2018 alipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Moja ya kumbukumbu na mfano wa kesi Kama Mwanasheria Mkuu, aliongoza mawakili wa serikali katika mashauri ya kihistoria, ikiwa ni pamoja na kesi maarufu dhidi ya Christopher Mtikila na masuala ya Bunge dhidi ya Waziri Mkuu Pinda, ambapo mahakama ilitoa uamuzi juu ya kinga ya wabunge bungeni.

Alipeperusha imani ya upeo wa mamlaka ya serikali na kuleta muundo wa uwakilishi wa kisheria.

Baada ya kuacha nafasi ya Mwanasheria Mkuu Februari 2018, aliteuliwa kama Jaji wa Mahakama Kuu na baadaye kuwa Mshauri wa Sheria kwa Rais.

Uteuzi wake wa hivi karibuni, umekuja ikiwa ni miezi michache tangu ateuliwe na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Januari 2025.

Stori: Elvan Stambuli



Prev Post Kitunda Walivyoadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika, na Kufanya Mjadala wa Kijamii
Next Post Shamrashamra Za Mapokezi Ya Rais Dkt. Samia Wilayani Busega, Simiyu – Picha
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook