Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kitunda Walivyoadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika, na Kufanya Mjadala wa Kijamii

  • 21
Scroll Down To Discover

Shirika lisilo la kiserikali la My Legacy la hapa Tanzania limeungana na wanajamii katika Kata ya Mzinga iliyopo Kitunda Dar katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika pamoja na Mhagawa wa Maarifa kwa kufanya mdahalo wa kijamii uliojadili suala la mabadiliko ya tabia ya nchi jinsi yanavyoathiri au kuleta ukatili wa kijinsia.

Tukio hilo lilianza kwa michezo ya watoto kwa michezo mbalimbali ikiwemo kucheza muziki, mpira, mashindano ya kuonesha vipaji katika uchoraji na mengineyo.

Katika burudani hiyo watoto hao walipata vinywaji kwa pamoja kama sehemu ya kuwafurahishwa watoto hao kwenye maadhimisho ya siku yao hiyo.

Katika hali ilionesha kujawa na furaha kwa watoto hao kwenye maadhimisho hayo walionesha vipaji vya hali ya juu katika mashindano ya kujibu maswali yaliyokuwa yakiwataka kueleza ufumbuzi cha wa changamoto za kimazingira ikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi.

Watoto hao walipoulizwa kama wanajua umuhimu wa kutunza mazingira walieleza kiufasaha mambo mbalimbali ikiwemo kupata hewa safi, mvua za mara kwa mara, kupata miti bora ya matunda, dawa za asili, malisho ya mifugo, mbao na mengineyo.

Hafla hiyo ilifunguliwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mzinga Kata ya Kitunda Nyaikoba Lyoba ambaye alikuwa miongoni mwa waliosimamia tukio hilo ambalo lilihudhuriwa na watu wazima pia.

Nyaikoba alifungua hafla hiyo na kuwakaribisha wananchi mbalimbali wakiwemo wadau My Legacy walioendesha maadhimisho hayo ambapo watu wazima nao walipata nafasi ya kushiriki mgawa wa maarifa ambao ni mdahalo wa kijamii na kupata nafasi ya kueleza yao ya moyoni kuhusiana na kero zilizopo kwenye jamii yao.

Amina All

Akizungumza na wanahabari katika maadhimisho hao, mratibu wa mipango kutoka Shirika la My Legacy, Amina Ally amesema lengo la maadhimisho hayo sambamba na Siku ya Mtoto wa Afrika ni kufanya mgahawa wa maarifa ambao ni mdahalo wa kijamii ambao uko kwenye program yao inayofadhiliwa na Ubalozi wa Highland

Amina ameendelea kusema;

“Leo tupo hapa kwa ajili ya kuongea na jamii kuhusiana na mabadiliko ya tabia ya nchi jinsi yanavyoathiri au kuleta ukatili wa kijinsia na kuathiri afya haki ya afya ya uzazi kwa makundi maalum ikiwemo wanawake, watoto na watu wenye uhitaji maalum.

“Kama tunavyojua mabadiliko ya tabia ya nchi mara nyingi huleta athari mbalimbali ikiwemo ukatili wa kijinsia.

“Tunapokata miti na kuharibu vyanzo vya maji tunaleta ukame lakini pia shida ya maji katika jamii, na mara nyingi wanaoathiriwa na shughuli hizi za kwenda kutafuta maji na kuni ni wanawake na watoto ambao huenda umbali mrefu kutafuta maji na kuni kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

“Hivyo basi wakiwa njiani wanajikuta katika hatari ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia haswa ikiwemo kubakwa na kulawitiwa au kushambuliwa na watu wenye dhamaira mbaya.

“Lakini tukirudi kuangalia athari hizo kwa wanawake na watoto haswa wakike wanajikuta wanashindwa kupata mahitaji maalum kwa mfano kunapokuwa na shida ya maji wanaoathirika zaidi ni watoto wa kike haswa wale waliopevuka.

“Hiyo ni kwasababu wanashindwa kujisafisha pale wanapokuwa katika siku zao za hedhi kwa kukosa maji safi na salama ya kujisafisha na mwisho wake kupata magonjwa magonjwa kama vile, U.T.I, fangasi na mengineyo ambayo baadae huweza kuwaletea matatizo mengine mengi makubwa.

“Jukumu letu kama wananchi hapa katika kata hii ya Mzinga lakini pia kwa jamii nzima ya Kitanzania ni kuhakikisha tunachukua jukumu la pamoja kuanzia sisi wenyewe kutafuta suluhisho la matatizo haya yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuhakikisha sasa tunapanda miti haswa sehemu ambazo tunaona udongo unamomonyoka. “Inachotakiwa ni kutunza vyanzo vyetu vya maji na kuhakikisha hatufanyi shughuli ambazo zinaweza kuharibu vyanzo hivyo kama vile, kulima, kulisha mifugo kwenye vyanzo hivyo na kuhakikisha kuwa maji yanakuwa safi na salama kwa watu wote kuweza kutumia.

“Lakini pia tunatakiwa kuziba mashimo yaliyopo barabarani ili mvua hata zinapokuja yasije kutokea maafa kama vile madimbwi makubwa kujaa na kuzuia huduma za usafiri hivyo hata ikitokea mama mjazimzito anataka kuwahishwa kituo cha afya kuwe mazingira magumu ya kumuwahisha. Hivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunalinda mazingira yetu”. Alimaliza kusema Amina.  

      

       



Prev Post Rais Dkt. Samia Amuapisha Jaji Mkuu Wa Mahakama Ya Tanzania – (Picha+Video)
Next Post Mfahamu Jaji Mkuu Mpya wa Tanzania George Masaju
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook