

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam SACP, Jumanne Muliro amesema Jeshi hilo limeanza kutekeleza sheria na kuhakikisha kuwa shughuli zilizokuwa zikifanyika katika Kanisa la Askofu Gwajima haziendelei kutokana na agizo la kusimamisha shughuli za kanisa hilo lililotolewa na Msajili wa Jumuiya za Kiraia
SACP. Muliro amesema Kama Askofu Gwajima anataka kuendelea na Shughuli za kanisa hilo afuate utaratibu wa kisheria ikiwa ni pamoja na kukata rufaa kwenye mamlaka za kisheria zilizowekwa na kibaikuwa ni kweli wamewakamata baadhi ya watu waliokuwa wanakaidi kufungwa kwa kanisa hilo kwa ajili ya kuzungumza nao kujua walikuwa na lengo gani
“Sisi jukumu letu ni kuona kwamba tunaitekeleza ile sheria na kusimamia kuona kwamba kilichoelekezwa na Ofisi ya Msajili basi kinatekelezeka na kutekelezwa kwake ni kutoendelea kufanya zile shughuli zilizokuwa zikifanyika katika kanisa la Askofu Gwajima” — Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro,
“Kama akitaka ziendelee kufanyika basi afuate utaratibu wa kisheria ikiwa ni pamoja na kukata rufaa kwenye mamlaka za kisheria zilizowekwa. Lakini kwa sasa tunatekeleza kile ambacho ni cha kisheria cha mamlaka iliyowasajili ambayo tayari imesitisha shughuli zao.” — SACP. Muliro,
“Wakati tukielekeza nini cha kufanya kulingana na maelekezo ya kisheria, kuna baadhi ya watu walikuwa wanafanya mambo ya kutoelewa, kwahiyo ikabidi tuwachukue na tunaendelea kuongea nao kujua kweli walikuwa hawaelewi kilichokuwa kinatekelezwa au walikuwa wanafanya tu kukataa kwa maana ya kutaka kusababisha fujo”— SACP. Muliro.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!