
Wanafunzi hao ni kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) walipata tuzo ya juu na tuzo ya mshindi wa pili. Shindano hilo lilihusisha mafunzo kwa vitendo, ubunifu na programu.
Wanafunzi waliopata tuzo ya juu ni Vida Mapunda (DIT), Joseph Msuya (UDSM), na Sigfrid Michael (UDOM). Katika nafasi ya pili, ikichukuliwa na Paul Nkingwa, Godlove Hipolite na Felix Kuluchumila wote kutoka UDOM.

Shindano hilo pia liliwatambua wakufunzi bora, ambapo Jumanne Ally kutoka (DIT) alipokea zawadi kuu na Dk. Alex Mongi kutoka (UDOM) akishika nafasi ya pili katika kitengo cha mfukunzi bora.
Shindano hilo linafanyika kila mwaka likilenga kuwapa wanafunzi ujuzi wa kufanya kazi katika mifumo ya kompyuta ikihusisha eneo la data na akili mnemba.
Pia linalenga kutoa matokeo ya kiubunifu ili kutatua changamoto za ulimwengu hasa katika sekta kama vile kilimo, huduma za afya na elimu.

Akizungumza baada ya kupata tuzo hiyo, mwanafunzi Vida Mapunda kutoka DIT alisema ushindi huo inawapa motisha ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kudhihirisha kuwa vipaji vya Watanzania vinaweza kushindana kimataifa.
Mkuu wa Chuo cha Teknolojia kutoka ndaki ya Habari na Mawasiliano (CoICT) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Baraka J. Maiseli- akipongeza uwekezaji wa serikali katika miundombinu ya TEHAMA.
Mkuu wa UDOM, Dk.Florence Rashidi alipongeza jitihada zinazofanywa na Huawei katika kusaidia sekta ya elimu kwa kuwawezesha wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya Tanzania kushiriki katika mafunzo ya vitendo na mashindano ya kimataifa.
Huu ni mwaka wa pili kwa wanafunzi kutoka Tanzania kufanya vizuri katika shindano hilo la TEHAMA, mwaka 2023-2024, wanafunzi watatu walitambuliwa kwa ufaulu mzuri.
Washiriki katika shindano hilo walitoka katika nchi 12 ambazo ni China, Brazil, Algeria, Morocco, Nigeria, Ufilipino, Singapore, na Serbia.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!