
Chama Cha Mapinduzi kimesema kitahakikisha kinayafanyia kazi maelekezo yote yalioelekezwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan katika kupitisha wagombea udiwani, Uwakilishi na Ubunge.
Pia chama hicho kimesema huu ni wakati sahihi wa kuwang’amua mapema ni wagombea gani waaminifu na Wazalendo kwa chama na Nchi.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo ,Khamis Mbeto Khamisi amesema maelekezo yakiotolewa na Mwenyekiti katika mkutano mkuu wa Taifa ni maagizo ya utekelezaji toka matawi hadi Taifa.
Mbeto alisema CCM kina uzoefu wa kutosha kutokana na tabia ya kukatwa kwa majina ya wanachama wenye utiifu na nidhamu kuachwa na kupendekezwa wagombea wasiokubalika katika jamii.
Alisema ni lazima sifa za kila mgombea zitokane na juhudi binafsi kwa chama ,uzalendo wake , historia na upendo alionao kwa nchi na chama kama vigezo na vipaumbele muhimu .
“Kwa ngazi zote toka matawi hadi Taifa tutayafanyia kazi maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM Rais samia .Tutakuwa makini kupitisha wagombea udiwani, uwakilishi na ubunge”Alisema Mbeto
Aidha, alisema lazima tukaangalie mwenendo wa kila mwanachama kabla ya uteuzi na kujua kama mgombea huyo ana nidhamu, mtii wa siasa, sera na itikadi ya chama anayeishi kimaadili na muaminifu .
“Tunampongeza sana Mwenyekiti wa chama Dk Samia kwa maelekezo yake kwetu. Tunakwenda kuyasismamia yote na kutenda haki bila kufanya kinyume chake”Alieleza
Pia Katibu huyo Mwenezi alisema kuteua au kupitisha wanachama mamluki , wasio na uzalendo kwa nchi na si wenye imani na sera zetu ,wamekuwa wakitupa lawama na majuto.
“Wakati wa TANU tulipoteza jimbo la mbulu .Alipitishwa Chifu Amri Dodo akaachwa Padri Herman Serwat aliyeongoza kura za maoni . Karatu akaachwa Dk Wilbroad Slaa akateuliwa Patric Qorro tukapoteza “Alieleza
Mbeto alisema hata Iringa Mjini Chama kilikipitisha jina la monica Mbega akaachwa Fredrik Mawakalebela aliyeongooza kura za maoni jimbo pia litatuondoka .
“Mwenyekiti ametukumbusha kwa nia njema tutende haki kwenye vikao vyyote vya maamuzi . Upendeleo, ubinafsi na rushwa uwe mwiko wa milele “Alisisitiza katibu huyo Mwenezi
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!