
Jeshi la Uganda limetangaza kusitisha mara moja ushirikiano wa kijeshi na Ujerumani, likimtuhumu balozi wa taifa hilo mjini Kampala, Mathias Schauer, kwa kushiriki katika “harakati za kuhujumu usalama wa taifa”.
Hatua hiyo imechochewa na kile serikali ya Uganda inadai kuwa ni mwenendo wa kuunga mkono upinzani na kuchochea uasi dhidi ya utawala wa Rais Yoweri Museveni.
Taarifa hiyo ilitolewa kupitia msemaji wa jeshi, Chris Magezi, ambaye aliandika kwenye mtandao wa X kuwa, “Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF) limeamua kusitisha mara moja shughuli zote za kijeshi na ulinzi na Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani.”Muda mfupi kabla ya taarifa hiyo rasmi, alituma ujumbe mkali kupitia mtandao wa X akisema, “Huyu balozi hafai kabisa kuiwakilisha Ujerumani nchini Uganda. Hii haina uhusiano na watu wa Ujerumani bali yeye kama mtu binafsi.”
Muhoozi, ambaye pia ni mtoto wa Rais Museveni na anayetajwa sana kuwa mrithi wa baba yake, anajulikana kwa matamshi yake ya uchokozi kwenye mitandao ya kijamii – akiwahi hata kuwatishia mabalozi wa mataifa ya Magharibi.
aarifa zinaeleza kuwa mvutano ulizidi baada ya balozi Schauer kutoa kauli kali katika mkutano kati ya ujumbe wa Umoja wa Ulaya na Jenerali Salim Saleh, kaka wa Rais Museveni, wiki iliyopita. Katika mkutano huo, Schauer alikosoa vitendo vya Muhoozi akisema vinaathiri taswira ya Uganda na vinavuruga uhusiano wa kikanda.
“Tunafahamu kuhusu sifa mbaya inayosababishwa na mkuu wa majeshi, na haonekani kushauriwa na mtu yeyote,” alisikika akisema kwa mujibu wa duru za karibu na mazungumzo hayo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!