Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Zaidi Ya Sh. Bilioni 28 Kujenga Kituo Cha Upandikizaji Figo Tanzania

  • 2
Scroll Down To Discover

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameshuhudia utiaji saini wa hati ya makubaliano ya ujenzi wa kituo kikubwa cha kupandikiza figo pamoja na utoaji mafunzo kwa madaktari bingwa ambacho kitakuwa ni kikubwa katika ukanda wa Jangwa la Sahara.

Kituo hicho ambacho kitajengwa kwenye Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma ni ushirikiano kati ya Shirika la Tiba la TOKUSHUKAI, Hospitali ya Benjamin Mkapa na Chuo Kikuu cha Dodoma na kinatarajia kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 28 ikiwa ni msaada usiokuwa na masharti yoyote.

Utiaji saini huo umefanyika Jumatatu, Mei 26, 2025 wakati kongamano la Biashara, Uwekezaji na Utalii lililowakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na wafanyabiashara na wawekezaji wa Japan katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Westin, Osaka, Japan, ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa Tanzania katika maonersho ya World Expo Osaka 2025. Kongamano hilo lilifunguliwa na Mheshimiwa Majaliwa.

Akizungumza baada ya utiaji saini huo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Profesa Abel Makubi amesema wamesaini makubaliano na shirika hilo linaloundwa na kundi la madaktari Wakijapan ambao wamekuwa wakisaidia utoaji na uboreshaji huduma za afya. “Hawa ni wadau wetu wa muda mrefu na walikuwa watu wa kwanza kusaidia utoaji wa huduma Dialysis katika hospitali ya Benjamin Mkapa.”

“MOU hii ambayo tumeisaini sasa hivi ni kwa ajili ya kujenga kituo cha umahiri katika upandikizaji figo kwenye eneo la Tanzania na Ukanda wa Jangwa la Sahara.”

Amesema mbali na ujenzi wa kituo hicho ambacho kitajengwa ndani ya hospitali ya Benjamin Mkapa na kutarajiwa kukamilika na kuanza kutoa huduma ndani ya miaka mitatu, pia Serikali ya Tanzania imejipanga kusaidia baadhi ya maeneo ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati. Ujenzi wa kituo hicho unarajiwa kuanza mwaka huu.



Prev Post Vijana Wa CCM Dar Washauri Askofu Gwajima ‘Atumbuliwe’ – Video
Next Post Uganda Yasitisha Ushirikiano Wa Kijeshi Na Ujerumani Kufuatia Tuuma Za Kuhujumu Usalama Wa Taifa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook