
Raia wa nchi mbili za Marekani na Ujerumani alikamatwa Jumapili kwa madai ya kujaribu kulipua ubalozi wa Marekani huko Tel Aviv, Israel, kulingana na wizara ya sheria.
Maafisa walisema walimkamata Joseph Neumayer, 28, katika uwanja wa ndege wa John F Kennedy mjini New York.
Alikuwa amerejeshwa na mamlaka ya Israel baada ya kupatikana na vifaa vya vilipuzi kwenye mkoba karibu na ubalozi huo.
Bw Neumeyer alifikishwa mahakamani Jumapili na anazuiliwa gerezani, wizara hiyo ilisema.
“Mshtakiwa huyu anashtakiwa kwa kupanga shambulio baya lililolenga ubalozi wetu nchini Israel, likitishia vifo kwa Wamarekani, na maisha ya Rais Trump,” Mwanasheria Mkuu wa Serikali Pamela Bondi alisema.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!