Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mwenyekiti wa NEC Jaji Mwambegele Akagua Maandalizi ya Uchaguzi Mbeya

  • 2
Scroll Down To Discover

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele, Septemba 19, 2025 ametembelea Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika majimbo ya Mbeya Mjini na Uyole, ili kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Katika ziara hiyo, Jaji Mwambegele alipokea taarifa ya maandalizi kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi wa halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya, na pia alikagua vifaa vya uchaguzi ambavyo tayari vimepokelewa katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Aidha, alipata fursa ya kutembelea kampeni za wagombea ubunge kutoka vyama vya CUF na CCM katika majimbo husika.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na Tume, Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 utafanyika Oktoba 29, 2025.

Tume imeendelea kuhimiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi, ikisisitiza kaulimbiu yake:
“Kura Yako, Haki Yako – Jitokeze Kupiga Kura.”



Prev Post Askofu Novatus Rugambwa Kuagwa Dar, Kuzikwa Bukoba
Next Post TLS Yatisha Maandamano ya Amani Nchi Nzima Kupinga Shambulio kwa Wakili
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook