Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Vodacom Yazindua Ofisi Mpya Kanda Ya Kaskazini Arusha

  • 31
Scroll Down To Discover

Mkuu wa kanda ya Kaskazini wa Vodacom Tanzania PLC Bw. George Venanty akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofisi mpya ya Kanda ya Kaskazini jijini Arusha. Tukio hilo lilihudhuriwa na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC Philip Besiimire, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Vodacom Tanzania Plc David Tarimo na Wafanyakazi wengine wa Vodacom Tanzania PLC

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC Philip Besiimire, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya Vodacom Tanzania Plc David Tarimo na Mkurugenzi wa Biashara Brigita Shirima wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wafanyakazi wengine wa Vodacom wakati wa uzinduzi wa ofisi ya Kanda ya Kaskazini na duka jipya la Vodacom jijini Arusha.

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC David Tarimo (wa pili kushoto), akimsikiliza Meneja wa maduka ya Rejareja wa kampuni hiyo Vanessa Mlawi kuhusu huduma mbalimbali za kidijitali wakati wa uzinduzi wa duka jipya pamoja na ofisi ya Vodacom kanda ya Kaskazini zilizoko katika jengo la PAPU jijini hapo uliofanyika jana, katika kusherehekea miaka 25 ya kampuni hiyo, inazidi kusogeza huduma zake kwa wateja kupitia njia mbalimbali ikiwemo za kidijitali, akisikiliza ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom, Philip Besiimire (mwenye kofia nyekundu).

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa ofisi ya kanda ya kaskazini na duka jipya viliyoko katika jengo la PAPU jijini Arusha.

Wateja wa muda mrefu wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kupokea zawadi, kama ishara ya shukrani kwa uaminifu wao kwa kampuni hiyo kwa kipindi cha miaka 25. Tukio hilo limefanyika jijini Arusha, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 25 ya kampuni hiyo.

The post Vodacom Yazindua Ofisi Mpya Kanda Ya Kaskazini Arusha appeared first on SwahiliTimes.



Prev Post THBUB  Yatoa Mafunzo Kwa Jeshi La Polisi Kuhusu  Haki Za Binadamu 
Next Post KISA SIMBA…..MASTAA YANGA WALAMBA MIL 200 ZA CHAP CHAP….DILI ZIMA LIKO HIZI….
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook