Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Paula Kajala Ateka Mitandao kwa Kauli Kuhusu Urembo Wake

  • 2
Scroll Down To Discover


Mwanamitindo na staa wa mitandao ya kijamii, Paula Kajala, amewavutia mashabiki wake baada ya kuweka ujumbe unaoonesha namna anavyojivunia muonekano wake, huku wengi wakimiminika kwenye ukurasa wake wa Instagram kutoa maoni yao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Paula aliandika, “You ever look at yourself & just think wow this face card is insane😌”, akimaanisha, je, huwa unajiangalia na kujikuta ukishangazwa na uzuri wa uso wako?

Kauli hiyo imepokelewa kwa maoni mbalimbali kutoka kwa mashabiki zake, wengi wao wakimsifia kwa urembo na muonekano wake, huku wengine wakitumia maneno ya kimahaba na emoji kuonesha namna walivyovutiwa na chapisho hilo.

Baadhi ya mashabiki walimwelezea Paula kama mwenye uzuri wa kipekee, huku mmoja akisema, “Facecard never to decline”, akimaanisha kuwa uzuri wake haupungui.

Shabiki mwingine aliandika, “Printing this caption on a tshirt and sending it to you as a present”, akionesha kufurahishwa na ujumbe huo kiasi cha kutaka kuuchapisha kwenye fulana na kumtumia kama zawadi.

Maoni mengine yalijaa sifa kama “Baddie”, “Gorgeous”na “Face card lethal”, huku baadhi ya mashabiki wakimhimiza Paula kufikiria kushiriki mashindano ya urembo ya kimataifa, ikiwemo Miss Grand International.

Hata hivyo, pamoja na sifa hizo, baadhi ya mashabiki walichangamsha mjadala kwa utani kuhusu matumizi ya vichujio vya picha, jambo lililoongeza maoni mbalimbali kwenye chapisho hilo.

The post Paula Kajala Ateka Mitandao kwa Kauli Kuhusu Urembo Wake appeared first on Global Publishers.



Prev Post Padri Afariki Baada ya Kuangukiwa na Msalaba Akiendesha Misa – Video
Next Post Carrick Aweka Wazi Hali ya Bruno Fernandes Baada ya Kiwango Kushuka
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook