
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Nishani ya Heshima ya Juu ya Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (The Grand Cordon) katika hafla iliyofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam, tarehe 14 Agosti 2025.
Nishani hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Baraza hilo kwa Kanda ya Afrika, Meja Jenerali Maikano Abdullahi kutoka Nigeria, ikiwa ni kutambua mchango na uongozi wa Rais Samia katika kuendeleza michezo ya kijeshi na kushirikisha Tanzania kikamilifu katika mashindano ya kimataifa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Meja Jenerali Abdullahi alisema tuzo hiyo ni ishara ya heshima kubwa na kuthamini juhudi za Tanzania katika kukuza mshikamano wa kijeshi kupitia michezo.
Kwa upande wake, Rais Samia alishukuru Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani kwa heshima hiyo na kusisitiza dhamira ya serikali kuendeleza michezo kama chombo cha kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na kuleta mshikamano wa kimataifa.



Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!