
Katika kuunga mkono hafla ya CCM Gala Dinner 2025 inayoendelea usiku huu katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, wadau wa sanaa na urembo wamejitokeza kutoa michango ya hali na mali.
Akitangaza kwa niaba ya wasanii, bila kubainisha tanzu wanazotoka, Steve Mengele maarufu kama Nyerere aliahidi kuchangia Sh milioni 10 kwa ajili ya kufanikisha tukio hilo maalum.
Kwa upande wake, mwanamitindo na mdau maarufu wa tasnia ya urembo, Millen Magese, naye alieleza dhamira yake ya kuchangia kiasi sawa cha Sh milioni 10, akisisitiza umuhimu wa mshikamano na mshikikamo katika kuchangia maendeleo kupitia tasnia mbalimbali.
Michango hiyo imeongeza hamasa miongoni mwa wageni waalikwa na wadau wengine waliokusanyika kwenye hafla hiyo ya kifahari, ambayo inalenga kuchangisha fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali inayoratibiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!