Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mwabukusi: Wananchi Wana Haki ya Kuhudhuria Kesi ya Lissu – Video

  • 5
Scroll Down To Discover

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, amesema ni haki ya kikatiba kwa wananchi kuhudhuria na kusikiliza mwenendo wa kesi, hivyo hawapaswi kuzuiwa kuingia mahakamani.

Amesema hayo leo nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar es Salaam, ambako inaendelea kusikilizwa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.

“Mahakama ni ya kiraia na si ya kijeshi. Raia wana haki ya kufika na kusikiliza kesi. Kama ukumbi ni mdogo, basi waingie wale wachache wanaoweza, lakini kwa amani. Kusiwe na vitisho au watu kujitutumua kana kwamba wana nafasi ya kipekee. Shauri linaposikilizwa mbele ya majaji, nguvu ya ushahidi ndilo jambo linalotakiwa kuongoza maamuzi ya mahakama,” alisema Mwabukusi.

Ameongeza kuwa ni muhimu kuzingatia misingi ya uwazi wa mahakama ili haki ionekane ikitendeka kwa pande zote mbili — mshtaki na mshtakiwa.



Prev Post Video: Dkt. Bashiru: Samia Atashinda Uchaguzi wa 2025 kwa Kishindo
Next Post Exim Bank Na GF Automobile Waingia Ushirikiano Kurahisisha Umiliki Wa Magari
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook