Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

RASMI….MABILIONI YA YANGA KUWEKWA HADHARANI….ENG HERSI KUANIKA KILA KITU….

  • 40
Scroll Down To Discover

WANACHAMA na viongozi wa Yanga wameitana jijii Dar es Salaam mwezi ujao kwa lengo la kujadili mambo yao kabla hata msimu mpya wa mashindano wa 2025-2026 haujaanza.

Wanayanga wanatarajiwa kukutana katika Mkutano Mkuu ulioitishwa na uongozi wa klabu hiyo utakaofanyika Septemba 7, 2025 kwenye Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam kuanzia saa nne asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said, mkutano huo unafanyika kwa mujibu wa Ibara ya 20 ya Katiba ya Yanga ya mwaka 2021 na utahusisha masuala mbalimbali ya kiutawala, kifedha na mipango ya maendeleo.

Taarifa hiyo imebainisha ajenda 10 zitakazojadiliwa, ikiwemo kufungua mkutano, uhakiki wa wajumbe, kuthibitisha ajenda, pamoja na kuthibitisha kumbukumbu za mkutano uliopita.

Ajenda nyingine ni kujadili masuala yaliyotokana na kumbukumbu hizo, kusikiliza hotuba ya Rais, kupokea na kujadili taarifa za kazi kutoka Kamati ya Utendaji, na kuthibitisha hesabu za fedha zilizokaguliwa za mwaka uliopita, ikiwemo mapato na matumizi ya klabu.

Aidha, wanachama watapewa nafasi ya kujadili na kuidhinisha bajeti ya mwaka unaofuata kabla ya kufungwa rasmi kwa mkutano huo.

The post RASMI….MABILIONI YA YANGA KUWEKWA HADHARANI….ENG HERSI KUANIKA KILA KITU…. appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post Rais Samia Kuchukua Fomu ya Urais Kesho
Next Post PAMOJA NA KUWA NO 5 KWA UBORA AFRIKA….CAF WAITUPA SIMBA LIGI YA ‘MCHANGANI’ ….
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook