Search
Sign In
2 Register
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Wanaocheza na Simba Kwenye Zoo Wapewa Tahadhari

  • 30
Scroll Down To Discover

Morogoro, 6 Agost 2025: Imekuwa kama fasheni flani iliyoibuka hivi karibuni hapa nchini kwa watu kutembelea kwenye bustani za wanyama pori (zoo) wakiwemo wanyama hatari kama Simba na wengineo na kucheza nao au kuwalisha vyakula wakiwa nao.

Katika matukio hayo tumewashuhudia watu wakipiga picha kuwachezea simba na kuwalisha chakula wanyama kama vile twiga na ndege wakubwa kama vile, mbuni, korongo na wengineo.

Akizungumza na mwandishi wetu kwenye banda la Dar es Salaam Zoo lililopo kwenye Maonesho ya Nanenane, Morogoro Afisa Wanyama pori Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama pori nchini (TAWA) aliyejitambulisha kwa jina la Proches Rongoma, amesema vitendo vya kucheza na mnyama kama simba ni hatari mno. Aliendelea kusema;

“Mnyama wa porini ni mnyama wa porini, hata ukimlea tangu utotoni na kumfundisha kuishi na binadamu baadae mnyama huyo kadili anavyozidi kukua anaweza kubadilika kitabia na kuwa na tabia zake za asili kama awapo msituni na hivyo kuweza kufanya lolote na hata kuwadhuru wanaomfuga.

Hivyo nawatahadharisha wanaokwenda zoo kucheza na simba wanaofugwa wafanye hivyo kwa tahadhari kwasababu kuna ushahidi wa simba wa kufugwa waliowahi kuwabadilikia binaadamu kwenye zoo. Alimaliza kusema afisa huyo.



Prev Post Airtel Africa Yasaini Ushirikiano Wa Kimkakati Wa Muda Mrefu Na Xtelify, Kitengo Cha Kidijitali Cha Airtel India
Next Post Job Ndugai Afariki Dunia leo
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook