
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ameibuka mshindi wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, kwa kupata kura 9,056 sawa na asilimia 97.63 ya kura halali zilizopigwa.
Akitangaza matokeo hayo leo Agosti 4, 2025, Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo alisema kuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo walikuwa 10,186, ambapo 9,276 (sawa na 91%) walijitokeza kupiga kura. Kura zilizoharibika zilikuwa 11, hivyo kura halali ni 9,265.
Makonda ameibuka mshindi kwa ushindi wa kishindo dhidi ya wagombea wengine sita waliokuwa wakigombea nafasi hiyo, akionesha kuungwa mkono kwa kiwango cha juu na wajumbe wa chama.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!