Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Benki ya Exim Tanzania Yazindua Elite Banking

  • 42
Scroll Down To Discover

Katika hatua ya kihistoria ya kuendeleza ahadi yake ya kuwapa wateja wake huduma bora, Exim Bank imebadilisha maana ya huduma za kibenki za kipekee kwa kuzindua rasmi huduma yake ya ‘Elite Banking’. Uzinduzi huu ulifanyika katika hafla iliyohudhuriwa na watu maalum katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, na kuwakutanisha wateja mashuhuri, wajumbe wa bodi, na washirika wa benki hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, Jaffari Matundu, alitoa shukrani za dhati kwa wateja wao ambao wamekuwa nguzo ya mafanikio ya benki hiyo kwa miaka mingi. “Elite Banking si huduma mpya tu, bali ni ishara ya dhamira yetu ya kuwaweka wateja wetu wa thamani katika kila tunachokifanya,” alisema Matundu.

Lengo la uzinduzi huu ni ‘Kutafsiri Upya Dhana ya Upekee’. Hii inaashiria mabadiliko kutoka kwenye dhana ya zamani ya kipekee inayotegemea hadhi, kwenda kwenye mtazamo wa kisasa unaozingatia umuhimu, kubinafsisha huduma, na kutoa fursa zenye hadhi. Matundu aliongeza, “Upekee huu mpya unahusu zaidi ya bidhaa za kipekee. Unaakisi dhamira yetu ya kutoa uzoefu wa kibinafsi, huduma maalum za kipekee, na huduma inayoweza kutambua mahitaji ya mteja na hata kuvuka matarajio yake.”

Kwa upande wake, Andrew Lyimo, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Rejareja katika Benki ya Exim Tanzania, alifafanua zaidi kuhusu huduma ya ‘Elite Banking’ na kutambulisha timu maalum ya usimamizi wa mahusiano ya wateja. Alisema kuwa huduma hii ni suluhisho kwa ajili ya mahitaji ya wateja wenye hadhi ya juu kwa kutoa urahisi na huduma iliyoboreshwa.

“Elite Banking imeundwa kuwasogezea wateja wetu ulimwengu wa huduma za kidigitali karibu zaidi popote walipo – kuanzia maeneo maalum ya kusubiria kwenye matawi yetu, huduma za kimataifa kwenye viwanja vya ndege kupitia Mastercard DragonPass, hadi suluhisho za kifedha zilizoboreshwa na faida za kipekee popote walipo na wakati wowote,” alifafanua Lyimo.

Uzinduzi huu unajengwa juu ya msingi imara uliowekwa na huduma ya ‘Preferred Banking’ iliyoanzishwa mwaka 2016, na sasa unavuka mipaka kwa kutoa suluhisho  za kibenki za kipekee kwa haraka na kwa ubora zaidi.

Kilele cha hafla hiyo ilikuwa ni uzinduzi wa huduma za Kadi za Mastercard World, zilizoundwa kwa ushirikiano na Mastercard. Huduma hii inajumuisha kadi tatu za hadhi ya juu: Mastercard World Debit Card (TZS), Mastercard World Debit Card (USD), na Mastercard World Credit Card.

Kadi hizi za kifahari zinafungua ulimwengu wa faida zisizo na kifani, zikiwapa wateja wa ‘Elite Banking’ fursa za kupata maeneo maalum ya kusubiria kwenye viwanja vya ndege kote duniani, huduma maalum za kipekee na huduma za usafiri wa kifahari, pamoja na bima kamili ya kusafiri inayojumuisha kila kitu kuanzia ajali hadi matibabu ya dharura. Wamiliki wa kadi hizi pia wanapata ulinzi thabiti wa manunuzi duniani kote, pamoja na zawadi za kipekee kwa ajili ya manunuzi, milo, usafiri, na burudani, zote zikiendeshwa na teknolojia ya kisasa ya malipo isiyotumia fedha taslimu.

Elsie Wachira-Kaguru, mwakilishi wa Mastercard – Tanzania, Burundi na Djibouti, alielezea kufurahishwa na ushirikiano huu. “Mastercard tuna furaha kuzindua huduma hizi mpya za kadi kwa kushirikiana na Exim Bank Tanzania, kufungua ulimwengu wa fursa za kipekee kwa wateja, huku tukilenga kuunda suluhisho zisizo na kifani. Tunajivunia kuendeleza mabadiliko ya kidijitali katika mfumo wa malipo nchini Tanzania kupitia ushirikiano wenye manufaa kama huu,” alisema.

Pamoja na mapinduzi ya huduma bora na za kisasa, ‘Elite Banking’ inafungua ukurasa mpya wa huduma zinazoendana na ulimwengu wa sasa wa kidijitali. Benki ya Exim Tanzania inabadilisha maana ya upekee kuwa jambo lenye mashiko, ikitoa suluhisho zilizojengwa juu ya uaminifu na teknolojia ili kuwawezesha wateja wake kufikia malengo yao makubwa na mapana.

Mwisho.

Kuhusu Exim Bank Tanzania

Exim Bank Tanzania ni mojawapo ya taasisi za kifedha zinazoongoza nchini, inayojulikana kwa uvumbuzi unaomlenga mteja, uaminifu, na kuvuka mipaka nje ya Tanzania. Benki inaendelea kuweka viwango vipya katika huduma za kisasa za kibenki ikiwa na huduma zinazokua kwa kasi.

Kuhusu Mastercard

Mastercard ni kampuni ya teknolojia ya kimataifa katika sekta ya malipo. Dira yake ni kuunganisha na kuwezesha uchumi jumuishi wa kidijitali unaowanufaisha wote, kila mahali, kwa kufanya miamala kuwa salama, rahisi, haraka, na yenye kufikiwa kwa urahisi.

The post Benki ya Exim Tanzania Yazindua Elite Banking appeared first on SwahiliTimes.



Prev Post Kituo cha Biashara Ubungo kuifanya Tanzania kitovu cha biashara na usafirishaji Afrika
Next Post Majambazi Watatu Wauawa na Polisi Kibondo, Kigoma
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook