

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 1, 2025, amefungua rasmi Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (East African Commercial and Logistics Centre – EACLC) kilichopo eneo la Ubungo, Dar es Salaam.
Kituo hicho kimelenga kuwa kiungo muhimu cha kuimarisha biashara, usafirishaji na usambazaji wa bidhaa ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, sambamba na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha kimkakati cha biashara katika kanda.
EACLC kinatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya usafirishaji, ajira, na uwekezaji, huku kikitoa huduma za kisasa kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi.



Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!