

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) leo Julai 28, 2025, limeshuhudia utiaji saini wa makubaliano ya pamoja kati ya taasisi sita kuhusu uendeshaji wa Bandari Kavu ya Kwala, hafla iliyofanyika Ukumbii wa Mikutano wa Bandari.
Makubaliano hayo yanalenga kuratibu uhamasishaji, uhifadhi na ukabidhiwaji wa mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Bandari Kavu ya Kwala, ikiwa ni hatua muhimu katika kuongeza ufanisi wa shughuli za bandari nchini.

Mkurugenzi Mkuu TASAC, Mohammed Salum amesema tukio hilo linaonesha mshikamano wa kiudhibiti na uwazi katika maandalizi ya nyaraka muhimu za uendeshaji wa bandari.
Amesema miongozo ya kiudhibiti inalenga kuhakikisha bandari kavu haziathiri shughuli za kiuchumi na kijamii jijini Dar es Salaam.
Amesema maeneo ya bandari kavu yanatakiwa kuwa na miundombinu ya kisasa ikiwemo reli na vifaa vya kutosha kuhudumia shehena, sambamba na kuwepo umbali wa angalau kilomita 30 kutoka bandari kuu ili kupunguza msongamano na kulinda usalama wa wakazi.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuunga mkono mpango huo, akisema kuwa uhamishaji wa mizigo kwenda Kwala ni fursa ya kuongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam.

Taasisi zilizotia saini ni pamoja na
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Chama cha Mawakala wa Meli Tanzania (TASAA), Kampuni ya DP World na Tanzania East Africa Gateway Terminal Limited (TEAGTL)


Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!