

Wakili Salim Bagachwa Abubakar, mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mzaliwa na mkazi wa kijiji cha Bugorora, kata ya Bugorora, wilayani Missenyi mkoani Kagera, ni mtiania wa Ubunge wa Jimbo la Missenyi kupitia CCM.
Wakili Salim Bagachwa siyo tu mwanasheria mwenye uzoefu mkubwa, bali ni mtumishi wa chama na jamii mwenye moyo wa kujitolea, uzalendo wa dhati, na dira ya maendeleo. Ameonyesha mfano wa kuigwa kwa kuunga mkono miradi ya chama, kujenga ofisi, na kutoa ardhi yake binafsi kwa maslahi ya chama.
Bagachwa, anasema ni muda sahihi wa kuwatumikia wananchi wa Missenyi kwa vitendo na dhamira ya kweli ya maendeleo huku akiwa na maono makubwa kwa jimbo hilo, na iwapo chama chake cha CCM kitampa ridhaa ya kupeprrusha bendera katika uchaguzi mkuu Oktoba 2025, kipaumbele chake kikubwa ni kuimarisha sekta ya elimu kwa wotena katika nyanja zote ili kuinua maisha ya wananchi, hasa vijana, kupitia kilimo chenye tija, biashara, ufugaji, utalii, uwekezaji wa ndani na nje.
Wakili Bagachwa anasema yeye kama mwananchi wa Missenyi anaelewa changamoto zilizopo lakini pia anaona fursa kubwa sana zilizopo na anamini Elimu bora na kwa kila mtu ni msingi wa maendeleo, lakini pia vijana haswa wanahitaji kusaidiwa katika kilimo cha mazao yenye thamani kama vanilla na kahawa ili waweze kujitegemea kiuchumi.
Na mpango huo unakamilika kwa kuwawezesha vijana na wananchi kupata elimu ya kilimo bora, pembejeo, masoko ya uhakika na mitaji kupitia vikundi na taasisi za kifedha ili kilimo kiwe na maana kwao.
Na haya ni baadhi ya mambo machache kwani wakili Bagachwa anayo mambo mengi ya kuwafanyia wananchi wa Missenyi iwapo chama kitampa ridhaa ya kupeperusha bandera ya CCM katika jimbo la Missenyi huku akiamini zaidi katika mshikamano na ushirikiano kati viongozi na wananchi.
#MissenyiKwanza #MisenyiniBagachwa2025 #SSH2025 #JeshilakijaniOktobatunatiki
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!