
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akitangaza kujiuzulu rasmi nafasi yake ya uwakilishi wa taifa hilo katika nchi ya Cuba, ukanda wa Karibe, Amerika ya Kati, pamoja na mataifa rafiki ya Colombia, Venezuela na Guyana.
Historia Fupi ya Utumishi wa Polepole
Humphrey Polepole amewahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya Serikali ya Tanzania, zikiwemo:
Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Novemba 2020 – Machi 2022).
Balozi wa Tanzania nchini Malawi (Machi 2022 – Aprili 2023).
Balozi wa Tanzania nchini Cuba (Aprili 2023 – Julai 2025).
Polepole pia alijulikana kwa muda mrefu kama mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, akiwa mmoja wa watetezi wakubwa wa maadili ya chama na utawala bora.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!