Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Kesi ya Kanisa la Ufufuo na Uzima Yaaahirishwa Hadi Julai 14, 2025 -Video

  • 12
Scroll Down To Discover

Dodoma, Tanzania – Kesi iliyofunguliwa na Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church (Ufufuo na Uzima) imeahirishwa hadi Julai 14, 2025, baada ya kushindwa kuanza kusikilizwa kama ilivyopangwa jana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.

Shauri hilo, linaloongozwa na Wakili Peter Kibatala kwa niaba ya kanisa hilo linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, linapinga zuio la serikali dhidi ya kuendelea kwa ibada na shughuli za kidini zinazodaiwa kukiuka masharti ya usajili.

Kwa mujibu wa Kibatala, wamewasilisha kesi namba 13189 ya mwaka 2025, wakiwashtaki Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na Msajili wa Taasisi za Kiraia, wakiomba mahakama itoe amri ya muda ya kuondoa zuio hilo hadi rufaa itakayosikilizwa baadaye itakapoamuliwa rasmi.

“Kesi hii ilitarajiwa kuanza leo, lakini kutokana na shughuli nyingi zilizokuwa zikifanyika mahakamani, imeahirishwa hadi Jumatatu ijayo, Julai 14, ambapo maombi yetu yataanza kusikilizwa pamoja na hoja nyingine za kisheria,” alisema Kibatala akizungumza na Nipashe Digital.

Shauri hilo limeibua hisia mbalimbali, hasa baada ya Maaskofu takriban 500 kujitokeza mahakamani Juni 13, 2025, kwa ajili ya kusikiliza maendeleo ya kesi hiyo kwa mara ya kwanza, wakionyesha mshikamano wao kwa uongozi wa kanisa hilo.

Hivi karibuni, mamlaka za serikali zilisitisha shughuli za kanisa hilo zikidai kuwa linaendesha ibada na kazi nyingine kinyume na masharti ya leseni ya usajili, hatua ambayo viongozi wa kanisa wamedai kuwa haikufuata misingi ya haki na utawala wa sheria.



Prev Post Serikali yatangaza ufadhili wa masomo kupitia Samia Scholarship
Next Post Watuhumiwa Watano Wakamatwa kwa Mauaji ya Mtumishi wa TASAF – Video
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook