
Rais wa Liberia Joseph Nyuma Boakai alitoa hotuba yenye mguso wa kipekee katika Mkutano wa Viongozi wa Afrika Magharibi uliofanyika katika Ikulu ya Marekani (White House) mnamo Julai 9, 2025, mkutano ulioandaliwa na Rais Donald Trump. Tukio hilo la nadra lilihudhuriwa pia na wakuu wa nchi kutoka Gabon, Guinea-Bissau, Mauritania, na Senegal.
Katika hotuba yake, Rais Boakai alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kibiashara, usalama wa kikanda, na utawala wa kidemokrasia, akitaja changamoto zinazowakabili wananchi wa Afrika Magharibi, huku akiomba Marekani isisite kusaidia juhudi za maendeleo barani humo hata katikati ya kupunguzwa kwa misaada ya Marekani kwa bara la Afrika.
Katika tukio hilo, Rais Donald Trump alimpongeza Boakai kwa kile alichokiita “Kiingereza kizuri sana,” kauli ambayo ilisababisha kicheko cha kutoeleweka kutoka kwa baadhi ya waalikwa, huku wengine wakiona kama ishara ya ukosefu wa uelewa kuhusu historia ya Liberia—nchi ambayo lugha rasmi ni Kiingereza tangu kuanzishwa kwake na watumwa waliorejea kutoka Marekani.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!