
Malabo, Julai 2, 2025 – Mahakama ya Juu ya Equatorial Guinea imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Uchunguzi wa Fedha, Baltasar Engonga, kifungo cha miaka 18 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa kadhaa ya kifisadi na matumizi mabaya ya madaraka.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Mahakama ya Malabo, Engonga amekutwa na hatia ya ubadhirifu wa zaidi ya Faranga bilioni 1, ambapo Faranga milioni 910 alizitia kibindoni kwa matumizi binafsi, hasa kwa anasa, wanawake na maisha ya kifahari yaliyo nje ya uwezo wa mshahara wake wa umma.
Mbali na tuhuma hizo, Engonga alihusishwa na:
Ubadhirifu wa mali ya umma
Uhusiano wa kingono kazini kinyume na maadili
Kushirikiana na maafisa wa zamani kuendesha mtandao wa kifisadi
Hata hivyo, Mahakama imebainisha kuwa hukumu hiyo haihusiani moja kwa moja na kashfa kubwa ya mwaka 2024 iliyohusisha video zaidi ya 400 za faragha zilizovuja na kuzua taharuki kimataifa.
Engonga, ambaye kwa miaka mingi alihusishwa na ngazi za juu za mamlaka nchini humo, amekuwa gumzo la kitaifa tangu ripoti za awali za uchunguzi zilipoanza kusambaa mwaka 2023. Hukumu hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti miongoni mwa wananchi na wachambuzi wa kisiasa, huku wengi wakitaka hatua zaidi dhidi ya “mtandao mkubwa wa kifisadi” ulioibuliwa na kesi hiyo.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!