Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

SIMBA & FADLU WAVIZIANA….MWENYEWE ATIA MSIMAMO HUU MPYA KUHUSU WACHEZAJI..

  • 40
Scroll Down To Discover

FADLU Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC amesema kuwa kwa msimu wa 2024/25 wamejitahidi kupambana na kufikia malengo licha ya kushindwa kutwaa ubingwa watafanya maboresho kwa msimu ujao.

Kuna asilimia chache kwa Fadlu kubaki ndani ya kikosi cha Simba SC msimu wa 2025/26. Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa Simba SC unafanya mazungumzo na kocha huyo ili aendelee kubaki ndani ya kikosi hicho.

Rekodi zinaonyesha kuwa baada ya kuongoza mechi 30 ni ushindi kwenye mechi 25, sare 3 na imepoteza mechi 2. Mechi hizo mbili ni Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC.

Kwenye mzunguko wa kwanza ilikuwa Simba SC 0-1 Yanga SC na mzunguko wa pili, Yanga SC 2-0 Simba SC. Ni mabao matatu Simba SC imefungwa huku Yanga SC ikiwa haijafungwa.

“Tulikuwa na msimu wenye ushindani mkubwa na kwa kiasi chake tumefikiwa malengo licha ya kutokufurahia yale ambayo yametokea. Kushindana na Yanga SC tukiwa na wachezaji ambao bado nwanazidi kuimarika inatupa nguvu kujipanga zaidi kwa wakati ujao.

“Tutazungumza na uongozi kuona namna yakufanya maboresho katika kikosi. Ninawapongeza mashabiki kutokana na kuwa nasi kwenye kila hatua.”

Mabingwa wa ligi ni Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi. Pointi zao kibindoni ni 82 huku safu ya ushambuliaji ikifunga mabao 83. Simba SC nafasi ya pili pointi 78 na safu ya ushambuliaji imefunga mabao 69.

The post SIMBA & FADLU WAVIZIANA….MWENYEWE ATIA MSIMAMO HUU MPYA KUHUSU WACHEZAJI.. appeared first on Soka La Bongo.



Prev Post Tumia Airtel Money na Ushinde Hisense TV, Samsung A25 na Safari ya Zanzibar
Next Post BASHIRI NA *149*10# USHINDE SAMSUNG A25….
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook