Katika nusu ya kwanza ya mwaka 2025, sekta ya benki nchini Tanzania imeonesha ukuaji mkubwa wa faida, huku benki ya NMB na CRDB Bank zikiendelea kushika nafasi za juu.
Takwimu zinaonyesha kuwa benki kubwa zimeendelea kudumisha nafasi zao za juu kwa mapato, zikionesha uimara wa mifumo ya usimamizi na ufanisi wa huduma kwa wateja.
Benki za kati na zile zinazokua zimeonyesha maendeleo ikiwa ni pamoja na ongezeko kubwa la faida kwa baadhi ya taasisi, ishara ya mikakati yenye mafanikio katika upanuzi wa huduma. Taasisi hizo zimeendelea kushindana kwa karibu, na hivyo kuongeza ushindani katika soko la kifedha nchini.
Hizi ni Benki 10 zenye faida kubwa zaidi Tanzania katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2025;
- CRDB Bank – TZS bilioni 346.45
- NBC Bank – TZS bilioni 73.76
- NMB Bank – TZS bilioni 358.57
- Tanzania Commercial Bank – TZS bilioni 17.84
- Stanbic Bank – TZS bilioni 68.68
- Standard Chartered – TZS bilioni 47.46
- Exim Bank – TZS bilioni 44.48
- Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) – TZS bilioni 34.08
- KCB Bank – TZS bilioni 29.42
- Azania Bank – TZS bilioni 27.73
Chanzo: The Citizen
The post Benki 10 zilizopata faida zaidi Tanzania nusu ya kwanza ya mwaka 2025 appeared first on SwahiliTimes.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!