

Dar es Salaam. Aliyekuwa Diwani wa Msasani na mfanyabiashara maarufu, Bw Luca Hakim Neghesti, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwania Ubunge wa Jimbo la Kigamboni.
Bw Neghest ni mjasiriamali mwenye mafanikio, mwanzilishi wa taasisi mbalimbali zikiwemo Bongo5 Media na amekuwa na mchango mkubwa katika masuala ya maendeleo katika Kata ya Msasani.
Bw Neghest ambaye ni mume wa Miss Tanzania wa mwaka 2005, Nancy Sumari ambaye aliitoa kimasomaso Tanzania kwa kushinda taji la Miss World Africa pia ana uzoefu mkubwa katika utumishi wa umma pamoja na sekta binafsi.
Mwisho…
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!