

Mkurugenzi wa kiwanda cha kusindika Kahama cha AMIMZA bw, Amir Hamza amechukua fomu ya kuomba ridhaa kwenye chama cha mapinduzi CCM kuwania Ubunge wa Jimbo la Bukoba mjini.

Devotha Daniel mapema leo hii amezulu katika ofisi za chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Kagera na kuchukua fomu ya kutia nia ya Ubunge wa viti maalumu mkoa wa Kagera.

Eng. Johnston Johansen Mutasingwa ni Mtanzania mzalendo, mtaalamu wa sekta ya ujenzi mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika usimamizi wa miradi ya maendeleo ya miundombinu kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), ambapo kwa sasa anahudumu kama Mkuu wa Kitengo cha Mizani, na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mipango kwa Mkoa wa Kagera amechukua fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Bukoba mjini.

Adv. Shabir Nuah Bigirwa wakili wa kujitegemea, Mwanasheria Mkuu mstaafu wa Bunge la vijana Tanzania na Mwanadiplomasia amechukua fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Bukoba mjini.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!