Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

SBL Yakabidhi Mradi Wa Maji Kwa Wakazi 14,000 Wa Kwadelo, Wilaya Ya Kondoa

  • 45
Scroll Down To Discover

Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mheshimiwa Dkt Ashantu Kijaji, akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa mradi wa maji wa Kwadelo, uliofadhiliwa na Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mheshimiwa Dkt Ashantu Kijaji, akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa mradi wa maji wa Kwadelo, uliofadhiliwa na Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL)

Dodoma, Tanzania – JunI 26, 2025: Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), kwa kushirikiana na shirika la Africa Community Advancement Initiative (Africai), imekamilisha na kuzindua rasmi Mradi wa Maji wa Kwadelo katika Wilaya ya Kondoa, Mkoa wa Dodoma, ikiwa ni uthibitisho wa dhamira ya SBL katika kuendeleza maendeleo endelevu na ustawi wa jamii kupitia upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.

Sherehe ya uzinduzi imehudhuriwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, ambaye alikuwa mgeni rasmi. Mradi huu mkubwa umegharimu kiasi cha shilingi milioni 292 na unatarajiwa kunufaisha zaidi ya wakazi 14,750wa Kata ya Kwadelo. Mradi huu umehusisha uwekaji wa pampu ya kisasa ya kuvuta maji (submersible pump), ujenzi wa nyumba ya mashine na tanki la kuhifadhi maji la saruji, mtandao mpana wa mabomba ya kusambaza maji, pamoja na vituo 11 vya kuchotea maji vinavyozalisha zaidi ya lita 107,000 za maji kwa siku.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mheshimiwa Dkt Ashantu Kijaji (kati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi wa maji wa Kwadelo, uliofadhiliwa na Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL)

Maji ni uhai. Mradi huu unaakisi imani yetu ya dhati kuwa upatikanaji endelevu wa maji ni msingi wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi. SBL tunajivunia kusaidia juhudi za serikali katika kuziba pengo la huduma ya maji katika jamii zenye uhitaji mkubwa,” alisema Obinna Anyalebechi, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL.

Tangu mwaka 2010, SBL imetekeleza jumla ya miradi 28 ya maji katika maeneo mbalimbali nchini, ikitoa huduma ya maji safi na salama bure kwa zaidi ya Watanzania milioni 2. Mradi wa Kwadelo ni sehemu ya programu ya muda mrefu ya SBL iitwayo “Water of Life”, na unalingana na malengo ya kampuni katika nyanja za Mazingira, Jamii na Utawala Bora (ESG), sambamba na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050.

Katika hotuba yake ya uzinduzi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji aliipongeza SBL kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto ya maji vijijini.

Ushirikiano wa aina hii ndio tunaouhitaji, ambapo sekta binafsi inakuwa sehemu ya kuleta mabadiliko ya kijamii. Maji siyo tu hitaji, bali ni heshima, afya, na fursa kwa jamii,” alisema Mhe. Kijaji.

Uzinduzi wa Mradi wa Maji wa Kwadelo si mwisho, bali ni mwanzo wa maisha bora na yenye afya kwa wakazi wa Kwadelo na maeneo ya jirani. SBL inasisitiza tena dhamira yake ya kuendelea kuwekeza kwenye miradi ya maji inayobadilisha maisha ya watu kote nchini Tanzania – ikisimamia upatikanaji wa maji, heshima ya binadamu, na maendeleo kwa wote.

SBL pia inatoa wito kwa washirika wa maendeleo, taasisi za serikali na sekta binafsi kushirikiana kwa pamoja katika kusaidia suluhisho za jamii zinazochochea ujenzi wa Tanzania bora zaidi.

MWISHO

Kuhusu SBL:

Ikianzishwa mwaka 1988 kama Associated Breweries, SBL ni kampuni ya pili kwa ukubwa wa uzalishaji wa bia nchini Tanzania, ikiwa na zaidi ya asilimia 25 ya soko kwa mujibu wa kiasi cha mauzo. SBL ina viwanda vitatu vya uzalishaji vilivyopo Dar es Salaam, Mwanza na Moshi. Tangu kuanzishwa rasmi mwaka 2002, SBL imeendelea kupanua wigo wa bidhaa zake kila mwaka. Ununuzi wa hisa nyingi kutoka EABL/Diageo mwaka 2010 umechochea uwekezaji mkubwa katika viwango vya kimataifa vya ubora na kutoa ajira zaidi kwa Watanzania.

Bidhaa za SBL zimepokea tuzo mbalimbali za kimataifa na ni pamoja na Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Serengeti Lemon, Pilsner Lager, Kibo Gold, Guinness Stout na Senator. Kampuni pia inauza vinywaji vya kimataifa kama Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon Gin, Captain Morgan Rum, na Baileys Irish Cream.

Kwa mawasiliano zaidi, wasiliana na:

Rispa Hatibu
Meneja Mawasiliano na Uendelevu, SBL
Simu: 0685 260 901
Barua pepe: Rispa.Hatibu@diageo.com

Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.



Prev Post Nilijaribu hii dawa ya mapenzi na mambo yangu yakabadilika usiku huohuo
Next Post Baadhi Ya Wagombea Waliochukua Fomu Ya Kuwania Ubunge Mkoa Wa Kagera
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook