

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Ruangwa mkoani Lindi, Kassim Majaliwa Majaliwa, amewashukuru wananchi wa Jimbo la Ruangwa kwa kuendelea kumuunga mkono na kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake. Ameeleza kuwa atarejea tena kuwania ubunge katika jimbo hilo.
Majaliwa ametoa kauli hiyo leo, Alhamisi, Juni 26, 2025, bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha hotuba ya kuhitimisha Mkutano wa 19 wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake na maelekezo yenye tija ambayo yameirahisisha kazi yake.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!