Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Serikali Yawarejesha Watanzania 42 Kutoka Nchini Iran Na Israel

  • 61
Scroll Down To Discover

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanikiwa kuwarejesha salama nchini Watanzania 42 kutoka nchini Israel na Iran kufuatia vita vilivyokuwa vikiendelea baina ya mataifa hayo mawili.

Akizungumza mara baada ya kuwapokea Watanzania hao kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amesema zoezi la kuwarejesha Watanzania wote salama nchini ni utekelezaji wa agizo maalumu la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha kwamba Watanzania wote waliopo katika mataifa hayo mawili wanarejeshwa nchini salama.

Aidha Balozi Shelukindo amesema Juni 25, 2025 wameingia Watanzania makundi mawili, kundi moja liliwasili mchana wa leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume na kwamba gharama zote za kuwarejesha Watanzania hao zimegharamiwa na serikali na kuongeza kuwa Watanzania wengine kutokea nchini Iran wanatarajiwa kuwasili nchini kesho Juni 26, 2025.



Prev Post Majaliwa Atangaza Kugombea Tena Ubunge Ruangwa 2025, Atoa Hotuba Ya Mwisho Bungeni – Video
Next Post NBC Yakabidhi Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu kwa Yanga
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook