
Maonesho ya nne ya Ubadilishanaji uzoefu na ajira kati ya China na Tanzania yanatarajiwa kufanyika tarehe 28 mwezi wa juni jijini Dar es salaam ambapo Makampuni takribani 100 yanayojihusisha katika sekta ya Ujenzi, utengenezaji bidhaa na huduma yenyewe yenye ubia na China na Tanzania yatashiriki Maonesho hayo.
Amezungumza hayo na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania Jumanne Sharobaro amesema kuwa Maonesho hayo yanalenga kuboresha ushirikiano kati ya sekta binafsi za biashara za China na Tanzania katika kuhakikisha Maendeleo ya ajira na rasilimali watu ambapo kupitia jukwaa hilo Watanzania watapata nafasi ya kufahamu mifumo itakayowawezesha kupata ajira.
Aidha mbali na kutoa ajira, Jumanne amesema maonesho hayo yanalenga kutoa mafunzo kwa kukuza taaluma na kuonesha miundo ya ufanyaji kazi kwa muda mrefu ambapo amewataka watu wote wenye sifa kuweza kuhudhuria maonesho hayo kwani maonesho hayo yatakuwa na fursa mbalimbali kwa ajili watanzania hususa ni wale wanatoaka kufanya kazi na makampuni ya China.
Tazama video kamili kupitia ukurasa wetu wa Facebook:
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!