Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Mhandisi Luoga Azindua Kampeni ya “Pika Smart” Kuhamasisha Upishi wa Kielektroniki Tanzania

  • 23
Scroll Down To Discover

Wa kwanza kushoto ni Mhandisi Henfried Byabato (Mkurugenzi wa Mipango, Utafiti na Maendeleo ya Biashara), na wa pili kushoto ni Dkt. Hawa Mwechaga, Mkurugenzi kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

Dar es Salaam, 13 Juni 2025. Wizara ya Nishati, kwa ushirikiano na Modern Energy Cooking Services (MECS) na UK International Development, wamezindua rasmiKampeni ya Kwanza ya Kitaifa ya Uhamasishaji wa Nishati ya Umem ya Kupikia(eCooking) nchini Tanzania. Mpango huu wa kihistoria ni sehemu muhimu ya Mpango waMECS wa kukuza na kusaidia nishati ya umeme unaofadhiliwa na UKAid, ambaounatekelezwa nchini Tanzania ili kuharakisha mabadiliko ya matumizi ya kuni na mkaakwenda kwenye matumizi ya umeme kwa shughuli za kupikia.

Kampeni hii inaunga mkono moja kwa moja Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi waKupikia wa 2024–2034, unaolenga kufikia asilimia 80 ya kaya kutumia mbinu safi za kupikia ifikapo 2034. Lengo la awali la kampeni hii ni kufikisha uelewa kuhusu faida za nishati ya umeme kupikia kwa asilimia 80 ya wakazi wa maeneo ya mijini na pembezonimwa miji kufikia Novemba 2025.

Akizungumza kabla ya uzinduzi huo, Mhe. Angellah Kairuki, Mshauri Maalum wa Rais waMasuala ya Nishati Safi ya Kupikia na Maendeleo ya Jamii, alisema:

Mabadiliko ya Tanzania kuelekea kupikia nishati safi si suala la nishati pekee, bali linagusaafya ya jamii, uhifadhi wa mazingira, uwezeshaji wa kiuchumi na usawa wa kijinsia. Kwa miongo mingi, jamii zetu zimekuwa zikibeba mzigo wa kutafuta kuni na mkaa kwa umbalimrefu, hali inayochangia magonjwa ya njia ya upumuaji, ukataji miti ovyo na umasikini. Kupitia kampeni hii ya kitaifa, tunapiga hatua jasiri kubadilisha namna Watanzaniawanavyopika, tukitumia mtandao wetu wa umeme unaokua na Mkakati mpya wa Nishati Safi ya Kupikia ili kukuza suluhisho za kisasa, nafuu na endelevu. Hili ni suala la kutoa nafasi yamaisha bora na yenye heshima zaidi kwa kila kaya, hususan wanawake na watoto.”

Dkt. Anna Clements, Mtafiti Mkuu wa Mpango wa MECS nchini Tanzania, aliongeza:

“Tuna furaha kuunga mkono Tanzania katika kuchunguza njia mpya za kupikia zinazotoaurahisi zaidi na mbadala safi, huku zikiheshimu mila na desturi za watu. Kadri umemeunavyopatikana zaidi na vifaa vinavyokuwa rahisi kutumia, kaya nyingi zaidi zitagunduafaida za njia za kisasa za kupikia zinazokidhi maisha ya kila siku. Kazi yetu ni kusaidiamazingira yatakayorahisisha uchaguzi huu na kuufanya uvutie zaidi.”

Kwa upande mwingine, Mhe. Marianne Young, Balozi Mkazi wa Uingereza nchiniTanzania, akizungumza kwa niaba ya UK International Development, ambaye ni mshirikamkuu, alisisitiza umuhimu wa kupikia nishati safi katika kufanikisha malengo ya maendeleoya kimataifa, hasa katika usawa wa kijinsia na mabadiliko ya tabianchi. Alieleza:

Kampeni hii ni hatua muhimu kwa malengo ya nishati na afya ya Tanzania. Inawahamasisha wananchi kufikiria namna mabadiliko madogo kwenye tabia za kupikiayanavyoweza kuleta manufaa makubwa, si kwa kubadili chakula chao, bali kwa kuwapatiachaguzi bora zaidi kwa familia zao na mazingira. Tunakaribisha kila mmojajamii, vyombo vya habari na wadaukushiriki kusambaza uelewa na kuunga mkono mabadilikohaya chanya.”

Kampeni hii itatekelezwa kwa kutumia mfumo wa mikakati ya miji, ikianza na Dar es Salaam na baadaye kuenea kwenye miji mingine mikuu. Kupitia maonesho ya wazi, mikutano ya kijamii, mitandao ya mabalozi wa ndani na kampeni za vyombo vya habari, kampeni hii itaonesha namna kupikia kwa umeme kunavyoweza kuwa salama zaidi, nafuu naendelevu kwa kaya za Kitanzania.

 

Mhandisi Innocent Luoga (Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Wizara ya Nishati) akizindua kampeni iitwayo Pika Smart kwa ajili ya kuhamasisha matumizi ya upishi wa kielektroniki (e-cooking) nchini Tanzania, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 13 Juni 2025.



Prev Post Mhandisi Luoga Azindua Kampeni ya “Pika Smart” Kuhamasisha Upishi wa Kielektroniki Tanzania
Next Post Mbinu ya kupambana na utapeli wa kila namna ni hii hapa
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook