Search
Sign In
2Your Cart
Your Cart 2 items
Subtotal : $1559

Chadema Yazuiwa Kufanya Shughuli za Siasa Hadi June 24

  • 50
Scroll Down To Discover

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepigwa marufuku kufanya shughuli zozote zile kiutendaji na oparesheni mpaka pale kesi ya msingi iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA itakaposikilizwa.

Jaji wa Mahakama Kuu Hamidu Mwanga anayesikiliza kesi hiyo namba 8323/2025 amesema zuio hilo la muda linakuja kufuatia maombi yaliyowasilishwa Mahakamani hapo na Mawakili wa waleta maombi wakiongozwa na Wakili Gido Thomas Simfukwe ambao waliiomba Mahakama kuweka zuio hilo hadi kesi ya msingi inayoanza kusikilizwa Juni 24, 2025 isikilizwe.

Kwenye kesi ya msingi waleta maombi wanadai kuwa CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo mgawanyo wa raslimali fedha n.k ambapo wakati wa kutangaza uamuzi huo, Jaji Mwanga amesema suala hilo ni la kisheria na halihitaji ubishani kwa sababu limefafanuliwa vyema kwenye sheria ya vyama vya siasa,

Wakati maamuzi hayo yanatolewa, upande wa utetezi (CHADEMA) haukuwa na mwakilishi yeyote Mahakamani, hiyo ni baada ya aliyekuwa Wakili wake Jebra Kambole kutangaza kujiondoa kwenye shauri hilo hatua iliyopelekea Mahakama kuendesha kesi kwa upande mmoja.



Prev Post Benki ya Absa Tanzania Yathibitisha Uwazi na Dhamira ya Ukuaji Katika Mkutano na Gavana wa BoT
Next Post CRDB Yafunguka Sakata La Yanga ‘hawadaiwi chochote’
Related Posts
Comments 0

    Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!

Leave A Comment
or

For faster login or register use your social account.

Connect with Facebook