
Benki ya CRDB imeingia makubaliano na Shule za Aga Khan kukusanya ada zinazolipwa na wazazi au walezi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hizo.
Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo ilifanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB ambapo CRDB iliongozwa na Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa na Shule za Aga Khan zikiwakilishwa na Afisa Mkuu wa Fedha, Karim Munir.
Raballa amesema makubaliano hayo waliyoingia na Shule za Aga Khan yatawezesha kukusanya ada zinazolipwa na wazazi au walezi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hizo.
‘Kupitia SimBanking, Internet Banking, CRDB Wakala, matawi, mitandao ya simu na TISS, wazazi sasa wanaweza kulipa ada kwa urahisi wakiwa mahali popote, kwa muda wowote’. alisema Raballa.
Raballa aliongeza kuwa ‘Huu ni mwendelezo wa dhamira yetu ya kuwekeza kwenye teknolojia inayogusa maisha ya kila mzazi, mwanafunzi na mwalimu hivyo kushiriki kuboresha elimu nchini’.
Hakuna maoni bado. Kuwa wa kwanza kuandika maoni!